30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ajali nyingine yaua mmoja, yajeruhi 28

air jordanNa Thomas Murugwa, Tabora
BASI la Kampuni ya Air Jordan lenye namba za usajili T 650 AQZ lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Arusha, limepata ajali katika Kijiji cha Ngonho, Kata ya Kitangili, Wilaya ya Nzega mkoani Tabora na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 28.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Jackline Liana, imemtaja aliyefariki dunia kwa jina moja la Emmanuel ambaye alikuwa ni fundi wa gari hilo.
Alisema sababu ya ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, ambaye alitokomea kusikojulikana baada ya kutokea ajali hiyo.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hosptali ya Wilaya ya Nzega, Erick Mbuguye, alisema alipokea majeruhi 28 ambapo kati yao
wanne hali zao ni mbaya huku mmoja akiwa amekatika mkono.
Alisema hali za majeruhi wengine zinaendelea vizuri, huku jitihada mbalimbali za kutoa huduma zikiendelea na kuongeza kuwa kwa wale watakaohitajika kupelekwa katika hospitali ya rufaa watapelekwa.
“Nimepokea majeruhi 28 na mwili mmoja, lakini tunaendelea kutoa huduma na kama ikihitajika kuwapeleka hospitali ya rufaa tutafanya hivyo, lakini hadi sasa bado na sidhani kama tutawapeleka hospitali ya rufaa, tunaendelea kuwapa huduma,”alisema Mbuguye.
Wakizungumza kwa nyakati majeruhi wamelaani baadhi ya waokoaji kutokana na kitendo chao cha kuwapora mali zao badala ya kuwaokoa.
Mmoja wa majeruhi hao, Frank Neto, ameliambia gazeti hili kuwa wananchi waishio pembezoni mwa barabara baadhi yao si waaminifu na hawana utu kutokana na kufanya vitendo vya kupora watu fedha na mizigo badala ya kuwaokoa pindi wanapopata ajali.
Neto akizungumzia chanzo cha ajali hiyo alisema ni mwendo kasi wa dereva ambaye aliyapita mabasi kadhaa huku akiwa katika eneo la kona ndipo gari hilo lilipomshinda na kujikuta likipinduka mara mbili.
“Tuseme ukweli dereva alikuwa mwendo kasi sana, alikuwa akiyapita mabasi kadhaa katika eneo hilo lenye kona ndipo gari likamshinda, mimi nilishtukia gari linakwenda kama mwendo wa nyoka, watu walipiga kelele, mwenye kuomba aliomba, mwenye kulia alilia,” alisimulia shuhuda huyo.
Taarifa ya Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani zilisema hadi juzi watu 866 walikuwa wamepoteza maisha na wengine 2,363 kujeruhiwa kati ya Januari hadi Machi mwaka huu huku zikiacha majeruhi lukuki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo alisema bado utambuzi wa majeruhi unaendelea na taarifa zaidi zitatolewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles