30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Airtel yakabidhi mil 20/- Nzega Mjini

airtelNa Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mfuko wake maalumu wa kusaidia jamii wa Airtel Fursa Tunakuwezesha, imekabidhi hundi ya Sh milioni 20 kwa Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), ikiwa ni mkakati wa kukamilisha dhamira yake ya kushirikiana na jamii katika kuinua vijana wa sehemu mbalimbali nchini.

Akikabidhi hundi hiyo jana, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colasa, alisema: “Airtel imejipanga kwa kuhakikisha vijana wanaendelea kunufaika na mradi wa Airtel Fursa kwa kuwapatia misaada ya kukamilisha mipango yao waliyoipanga kwa kupunguza changamoto walizonazo, ikiwemo ya ukosefu wa ajira na  mtaji ili watimize malengo yao katika biashara.

“Tunaamini kupitia ushirika wetu na Mbuge Nzega Mheshimiwa Hussein Bashe, Mfuko wa  Nzega Trust Fund utasaidia wananchi ndani ya vijiji 21 katika jimbo hilo ambapo malengo yetu ni kufanya mradi huu kuwa endelevu hata kwa majimbo mengine nchini,” alisema Colasa.

Kwa upande wake, Bashe aliishukuru Airtel na kuahidi kusimamia mradi huo wa ukopeshaji kwa ajili ya kuweza kuinua vipato vya wananchi wa Nzega kama ilivyokusudiwa.

“Nitoe wito kwa wananchi wote wenye malengo ya kujiendeleza wajisajili katika Mfuko wetu wa Nzega Trust Fund niliouanzisha kwa ajili ya kuhakikisha tunaungana na wadau wenye nia ya kusaidia jamii kama Airtel Fursa ili kupunguza changamoto za maendeleo kwa wananchi hasa kwa  wanaokosa mitaji ya kuendesha miradi yao mbalimbali.

“Airtel tayari wamezikabidhi pesa hizi kwangu ambazo tutazikopesha kwenu kwa riba ya asilimia 1.5 pale unaporejesha na faida inayopatikana bado itaendelea kuwasaidia vijana wengine watakaotaka kukopa,” alisema Bashe.

Mradi wa Airtel Fursa umeanzishwa Mei mwaka jana na tayari umewafikia vijana zaidi ya 5,000 kutoka katika mikoa 10 nchini, ikiwa ni pamoja na vijana zaidi ya 100 waliowezeshwa kwa kupewa mitaji na vitendea kazi  mbalimbali.

Programu hii kati ya Airtel na Nzega Trust Fund chini ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, Hussein Bashe, itawawezesha  zaidi ya  wajasiriamali 350 kunufaika na mikopo kupitia huduma ya Airtel Money.

Mikopo hiyo itatolewa kwa kikundi kilichoundwa na vijana watano ambao watapewa  mtaji kati ya Sh 100,000 hadi milioni moja kulingana na mahitaji yao.

Sambamba na mikopo hiyo, vikundi vya wajasiriamali vitaendelea kupewa mafunzo ya ujasiriamali, ikiwa ni pamoja na namna ya kuendesha vikundi pamoja na jinsi ya kutafuta soko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles