23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Ahukumiwa kunyongwa kwa kuua na kupora chupa ya chai

Malima Lubasha -Musoma

 MAHAKAMA Kuu Kanda ya Musoma, imemuhukumu kunyongwa hadi kufa mkazi wa Kijiji cha Kibubwa, Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Waryoba Elias baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki kumuua Chacha Ibuga usiku wa kuamkia Novemba mosi, 2017.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, John Kayohoza, alimkumbushia mshtakiwa shtaka lililokuwa linamkabili katika kesi hiyo namba 33/2019.

Jaji Kayohoza akisoma mazingira ya kesi na ushahidi wa mashahidi watano, ilielezwa Novemba mosi, 2017 saa 6.00 usiku, mshtakiwa akiwa na wenzake watano ambao hawajafahamika, wakiwa na tochi mbili na mapanga, walivamia nyumbani kwa Chacha Isoye Ibuga.

Ilielezwa wakati Ibuga akiwa ndani, kabla ya kuvamiwa alisikia mbwa wake anabweka na kuamua kutoka nje kuona kuna nini na ghafla watu hao walimshambulia kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili, hasa kichwani na kupiga kelele kuomba msaada, ndipo mke wake, Lucy Lukondo alilazimika kutoka kwa lengo la kumsaidia.

Wakati Lucy anatoka ndani, alikutana na watu watatu na kumzuia na kumlazimisha kuingia ndani kumtaka awape fedha.

Kwamba mshtakiwa huyo kwa kushirikana na wenzake walifanya upekuzi ndani ya chumba alichokuwa analala marehemu na mke wake na kufanikiwa kupora fedha taslimu Sh milioni moja, chupa moja ya chai na simu moja ya mkononi.

Imeelezwa miongoni mwa watu walioingia ndani, aliyekuwa mmoja wa washtakiwa alikuwa ni jirani yao ambaye anamwita marehemu mjomba.

Watu hao baada ya kutekeleza ukatili huo, walitoweka na kwenda kusikojulikana huku majeruhi Ibuga akipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Butiama ambako baadaye alifariki dunia na baada ya siku kadhaa mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles