31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kulawiti mtoto wa miaka 11

BEATRICE MOSSES, MANYARA

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Rift valley English Medium and Primary School iliyopo Babati mjini mkoani Manyara, Charles Msele (32), amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kulawiti.

Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Manyara, Simon Kobero, amesema adhabu hiyo imetolewa baada ya mtuhumiwa kutiwa hatiani.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo September 28 mwaka jana.

“Mtuhumiwa alimlawiti mtoto wa kiume wa miaka 11 mwanafunzi wa darasa la tano wa shule hiyo ambapo tukio hilo lilitokea shuleni hapo kwenye bweni la watoto wa kiume,”

Imeelezwa kuwa mtuhumiwa alimuita  mtoto huyo bwenini na baada ya  hapo na yeye alienda akiwa na vilainishi aina ya femo pamoja na mafuta ya mgando aina ya baby soft ambapo baada ya kufika bwenini mtuhumiwa alimpaka mafuta hayo kwenye  sehemu za haja kubwa kisha yeye kujipaka sehemu zake za siri na kumlawiti.

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani Oktoba 8, mwaka jana kwa mara ya kwanza ambapo alisomewa shtaka lake na kukana,  baada ya kukana kosa hilo shauri liliendelea kwa hatua ya usikilizwaji. 

Upande wa mashtaka ulisema kwa kuwa mshtakiwa ametiwa hatiani, mwendesha mashtaka Wakili wa serikali Petro Ngassa, aliomba mtuhumiwa apewe adhabu kali pamoja na kutoa fidia kwa muhanga kutokana na kitendo alichokifanya.

Mtuhumiwa aliomba apunguziwe adhabu pasipo kutoa sababu yoyote na ndipo mahakama ilipomuhukumu kifungo cha maisha jela lakini pia kuchapwa viboko vinne kwenye makalio na kulipa fidia kwa mhanga kiasi cha sh. milioni tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles