30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

AGIZO LA NEC KWA WAKUU WA MIKOA, WILAYA LITEKELEZWE

 

KATIKA toleo la jana la gazeti hili, tulichapisha habari kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuagiza wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kujiepusha na masuala ya kisiasa.

NEC imewaandikia wakuu wa mikoa ambao hivi sasa mikoa yao inakabiliwa na kampeni za uchaguzi wa marudio wa ubunge mwezi huu na mwezi ujao.

Majimbo ambayo yanatarajiwa kufanya uchaguzi na  mikoa yao kwenye  mabano ni pamoja na Siha (Kilimanjaro), Kinondoni (Dar es Salaam), Songea Mjini ( Ruvuma) na Singida Kaskazini (Singida).

Tunaamini uamuzi  huu wa tume umekuja wakati mzuri ambapo watendaji wa Serikali wanapaswa kuacha kujihusisha na uchaguzi hizi, kwa sababu wanasimamia majukumu mengi  na makubwa ya Serikali.

Pamoja na ukweli kwamba wakuu wa mikoa, wilaya na wakugurenzi wanatokana na chama tawala, lakini tiketi ya kuwafanya waingie moja kwa moja kwenye uchaguzi huu jambo ambalo linaweza kuzuia malalamiko mengi kutoka kwa vyama vingine vinavyoshiriki uchaguzi huo.

Tunakubaliana na uamuzi huu uliotolewa na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima kwamba ili kuhakikisha kila chama kinatimiza wajibu wake, ni vizuri viongozi wa Serikali wakakaa kando kwa nia njema kabisa.

Tunaamini kila yule aliyendikiwa baru hii, atatambua mipaka yake ya kazi ili aiingize siasa na utendaji kazi wa kila siku ambao kwa namna moja au nyingine anaweza kuathiri  majukumu yake.

Kwa vile viongozi hawa  wakuu wa mikoa na wilaya ndiyo wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama kwenye maeneo yao, basi wahakikishe wanasimamia kwa nguvu zote suala zima la amani ili mwisho wa siku wananchi wa maeneo hayo waweza kuchagua mwakilishi wao bila usumbufu.

Tunasema hivyo kwa sababu tukiamini sehemu yoyote ambayo usalama uanapokuwa mdogo hakuna jambo la maendeleo linaloweza kufanyika. Kwa msingi huo tuna imani kubwa kuwa viongozi hawa watalisimamia jambo hili na kulipa uzito wa aina yake.

Lakini pia tunawakumbukusha wakuu wa mikoa na wilaya wote ambao uchaguzi huu unafanyika majimboni mwao, kuhakikisha haki inatendeka na kuachana na michezo michafu ambayo imekuwa ikalalamikiwa  na vyama vingine vinavyoshiriki  uchaguzi.

Moja ya kilio kikubwa ambacho hata juzi viongozi wa vyama vya siasa walipokutana na NEC mjini  Dar es Salaam na kusema waziwazi ni kamatakamata ya viongizi ambayo imekuwa ikifanywa na polisi.

Kama tulivyoeleza hapo juu ya viongozi hao kuwa makini, pia tunaliasa Jeshi la Polisi kuhakikisha linasimamia ulinzi na usalama kwenye maeneo hayo kwa kuzingatia sheria  na si kuonyesha upendeleo.

Tunaamini kwa kufanya hivyo, vilio na maneno mengi ya malalamiko  yanayotolewa kila siku kamwe hatutayasikia.

Tunamalizia kwa kusema viongozi hawa wanapaswa kutumia muda wao mwingi kutatua kero zinazowakabili wananchi kama ambavyo Rais Dk. John Magufuli amekuwa akisisitiza mara kwa mara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles