24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Afya ya Askofu Ruwaichi yaimarika

Aveline Kitomary, Dar es Salaam

Hali ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Katoliki Dar es salaam, Mhashamu Yuda Ruwaichi inaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa ubongo jana.

Daktari Bingwa wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Profesa Joseph Kahamba anasema Askofu Ruwaichi alikutwa na tatizo la damu kuvuja kwenye ubongo linaloitwa Chronic Subdural Haematoma.

“Aliletwa alikuwa tayari alifanyiwa upasuaji KCMC wao waliona anahitaji matibabu zaidi hivyo alivyo kuja alifanyiwa upasuaji na madaktari bingwa watatu.

“Hata hivyo timu ya wahudumu wa afya saba wako wanampatia matibabu lakini mpaka sasa hali yake inaendelea vizuri,anajitambua, anaongea na pia anaeleza hivyo kwa ujumla hali yake inaendelea vizuri,” amesema Profesa Kahamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles