27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Afrika Kusini yaungana na Burundi kujitoa ICC

Rais wa Burundi, Piere Nkurunziza
Rais wa Burundi, Piere Nkurunziza

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

SIKU nne baada ya Rais wa Burundi, Piere Nkurunziza kusaini sheria ya kuiondoa nchi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, Afrika Kusini imeanzisha mchakato wa kujiondoa kutoka uanachama wa mahakama hiyo.

Afrika Kusini imechukua uamuzi wa kuanzisha mchakato huo kufuatia shinikizo ililokumbana nalo mwaka jana kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita za kuitaka imkamate Rais wa Sudan, Omar al Bashir, wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Johannesburg.

Sakata hilo lilitokea Septemba, mwaka jana, ambapo Mahakama Kuu ya Afrika Kusini iliinyima serikali ya nchi hiyo ruhusa ya kukata rufaa uamuzi ulioishutumu kwa kukosa kumkamata Omar al Bashir aliposhiriki mkutano huo Juni mwaka 2015.

Serikali ya Afrika Kusini ilijaribu kukata rufaa uamuzi wa Mahakama Kuu, ikisema Al Bashir alikuwa na kinga ya urais kwa sababu yeye ni kiongozi wa taifa. Lakini Jaji Hans Fabricius alipinga suala hilo na kusema rufaa hiyo haiwezi kufanikisha chochote.

“Afrika Kusini ni mwanachama wa Mkataba wa Roma uliounda Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita na mkataba huo unabatilisha sheria zote ambazo huenda zingempa kinga Bashir asikamatwe na kushtakiwa,” amesema Jaji Hans Fabricius.

Kiongozi huyo wa Sudan amekuwa akisakwa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki na makosa ya uhalifu wa kivita Darfur.

Omar al Bashir, aliyechukua mamlaka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989, amekuwa akisakwa na Mahakama ya ICC kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki na makosa ya uhalifu wa kivita katika Jimbo la Darfur, madai ambayo Bashir amekanusha.

Itafahamika kwamba nchi nyingi za Afrika zinailaumu ICC kwa kuzilenga zaidi nchi za Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles