31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

AFB wapokea dola mil 20 kupanua uwekezaji

afbNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Huduma za Kifedha ya AFB inayojihusisha na kutoa ushauri na huduma za kifedha kwa wajasiriamali imeingia mkataba wa dola milioni 20 za Marekani na Kampuni ya GEMCORP, inayojihusisha na uwekezaji wenye mtazamo wa masoko.

Akizungumzia mkataba huo jana, Mkurugenzi wa AFB, Karl Westvig, alisema amefarijika kuingia mkataba huo uliokuja wakati muafaka kwao.

“Uwekezaji huu wenye mantiki kutoka kwa GEMCORP utatoa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

“Kwa sasa tupo pia katika mataifa ya Ghana, Kenya, Zambia na Tanzania, huku tukiwa na mpango wa kujitanua katika nchi nyingine za Afrika ifikapo mwaka 2020, ikiwa na bidhaa zenye ubunifu na ufumbuzi wa hali juu wenye kukidhi vigezo vyote sokoni,” alisema Karl.

Alisema kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia (WB), zaidi ya watu milioni 400 waliopo Kusini mwa Jangwa la Sahara bado wanafanya shughuli zao nje ya mfumo rasmi wa kifedha.

“Tuna lengo la kutoa huduma rahisi za kifedha kwa watu ambao wamekuwa nje ya mfumo, kwa kufanya hivyo kutawarahisishia kuboresha maisha yao,” alisema Karl.

Akizungumzia uwekezaji huo, Mkurugenzi wa GEMCORP, Atanas Bostandjiev, alisema huduma za fedha ni sekta muhimu kwa mustakabali kwao na wamekuwa wakiangalia hasa soko la Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles