23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

AFARIKI AKIFANYIWA UPASUAJI WA KUONGEZA MAKALIO

 

ISTANBUL, Uturuki


Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 23, anaripotiwa kufariki dunia, baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio kwa lugha ya kitaalamu Brazilian Butt Lift.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, mwanamke huyo, Leah Cambridge kutoka mjini Leeds nchini England, alikutwa na umauti huo, baada ya kusafiri  hadi nchini hapa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huo, lakini wakati kazi hiyo ikiendelea  alipata mishtuko mitatu ya moyo.

Mwenzake ambaye aliongozana naye, Scott Franks, aliliambia gazeti la The Sun kwamba mwanamke huyo akifariki  baada ya kudungwa sindano ya ganzi katika kliniki moja iliyopo katika  mji wa Izmir uliopo Magharibi mwa  nchi hii.

“Mrembo huyo alikubali kufanya upasuaji ughaibuni ambapo ni bei nafuu ikilinganishwa na Uingereza baada ya kukerwa na mafuta mengi katika sehemu yake ya tumbo baada ya kupata watoto,” alisema Frank.

Wakizungumza na gazeti hilo, majirani zake walimtaja mwanamke huyo kuwa alikuwa anayevutia na wakasema kwamba wanaamini alienda kufanyiwa upasuaji huo mwezi uliopita bila kumshauri mpenzi wake.

Hata hivyo, Cambridge si mwanamke wa kwanza kutoka Uingereza  ambaye amewahi kuwa na hamu ya kuwa na makalio ya kuvutia kupoteza maisha  akiwa ughaibuni.

Mwanamke mwingine ambaye aliwahi kukutana na kifo ni Joy Williams ambaye alifanyiwa upasuaji kama huo, Oktoba 2014   mjini  Bangkok  nchini Thailand, lakini  vidonda vyake vilipata maambukizi na mwanamke huyo ambaye alikuwa na umri wa miaka  24, alifariki  wakati akidungwa sindano ya ganzi.

Miaka mitatu kabla  ya kutokea kifo hicho, Claudia Aderotimi, mwenye umri wa miaka 20 kutoka katika mji wa Hackney, uliopo Mashariki mwa Jiji la London alifariki  akiwa hotelini nchini Marekani wakati akipatiwa  matibabu ya vidonda vya kujiongeza makalio yake.

Mmoja wa madaktari ambao wanafanya kazi hiyo ya upasuaji, Bryan Mayou, alisema licha ya upasuaji huo wa kuongeza makalio kutoonekana kuwa hatari, lakini ni tishio kama aina nyingine zozote za upasuaji.

“Hatari hiyo inatokana na kuwa  upasuaji huo kufanywa na madaktari ambao hawajahitimu, nje ya hospitali  bila kuwa na maelezo ya jinsi ya kujichunga baada ya matibabu hayo kufanywa,” alisema Daktari  Mayou, ambaye ni  mwanachama wa muungano wa madaktari wa upasuaji nchini Uingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles