30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

AFA BAADA YA KUFAKAMIA POMBE YA KIENYEJI

26196_1426102131470_1200297381_31238600_4999062_n

NA SHEILA KATIKULA-MWANZA

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Bahati Mbula (43) mkazi wa Kanindo Kata ya Kishiri amefariki dunia kwenye mkesha wa mwaka mpya baada ya kudaiwa kunywa pombe za kienyeji kupita kiasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema hilo ni tukio pekee lililotokea katika mkesha wa mwaka mpya mkoani Mwanza.

“Nimepata taarifa moja tu ya mtu mmoja kufariki huko Kanindo, marehemu huyo anadaiwa kunywa kwa kuchanganya pombe za aina nyingi za kienyeji.

“Nimeambiwa marehemu huyo alitoka eneo la Sawa Kata ya Lwahnima na kwenda kunywa huko Kanindo, sasa usiku huo wenzake walidhani ameondoka kurudi kwao kumbe alikuwa ameanguka  njiani karibu na pale alipokuwa akinywa pombe hiyo,” alisema Kamanda Msangi.

Alisema Jeshi la Polisi linafuatilia kwa uchunguzi zaidi kama alikuwa anaumwa au kuna kitu kingine.

“Tuliwaambia wananchi washerekee  mwaka mpya bila kuleta madhara yoyote ikiwamo kuchoma moto matairi, kuendesha magari ovyo,  kurusha mawe nadhani watu walizingatia ndiyo maana hata matukio ya uhalifu hayakuwapo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles