24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

ACT KUJADILI KUNG’OKA SAMSON MWIGAMBA

NA TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM



KAMATI ya Uongozi ya Chama Cha ACT- Wazalendo inatarajia kukutana kesho kujadili kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, Samson Mwigamba.

Mwigamba alijiuzulu wadhifa wake ndani ya chama kwa madai kuwa mambo hayaendi sawa katika chama hicho na hivyo kuamua kuwa mwanachama wa kawaida.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu alisema kamati ya uongozi itakujana kesho kujadili kwa kina hatua ya kiongozi huyo mwasisi wa chama hicho kung’atuka.

“Kujiuzulu kwa Mwigamba ni utashi wake na sisi kama chama tumekubaliana na uamuzi wake… tunaheshimu uamuzi wake na si kumshinikiza na tunatambua kwamba Mwigamba bado ni mwanachama wa ACT-Wazalendo,” alisema Shaibu.

Alisema chama hicho kitaendelea kupambana na kupigania haki za raia na misingi ya demokrasia nchini.
Akizungumzia upatikanaji wa soko la zao la mbaazi, Shaibu alisema Agosti 5, mwaka huu serikali ya India ambayo ndiyo wanunuzi wakubwa wa zao hilo imefungia uagizwaji wa mbaazi kutoka nje ya nchi hiyo.

Alisema zuio hilo halikuistahili Tanzania kwa kuwa imekuwa na uhusiano wa undugu, kuwa na mkataba nayo wa biashara na kwamba wao waliwahakikishia wakulima soko la uhakika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles