ABIRIA 109 WAACHILIWA HURU KWENYE NDEGE ILIYOTEKWA NYARA NCHINI LIBYA

0
610

ndege-ya-libya

Ndege moja ya Libya iliyoripotiwa kutekwa nyara ikiwa kwenye safari ya ndani ya nchi imetua nchini Malta na abiria 109 waachiliwa huru.

Lakini pia waliosalia kwenye ndege ni watekaji hao wawili pamoja na wahudumu wa ndege hiyo.

Ndege hiyo aina ya Airbus A320 ya shirika la ndege la serikali ya Libya, Afriqiyah, ilikuwa na abiria 118 wakati inatekwa.

Imeripotiwa kuwa, tukio hilo limefanywa na watekaji nyara wawili ambao walitishia kuilipua ndege hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa ikitoka mji wa Sebha kusini magharibi mwa Libya ikielekea mji mkuu Tripoli kabla ya kuelekezwa nchini Malta na kutua hapo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here