MSHINDI wa tuzo ya Black Entertainment Television ‘BET’, Lupita Nyong’o, anatarajia kung’aa kwenye filamu mpya ya ‘Star War’ ambayo inatarajiwa kuachiwa Desemba 18, mwaka huu.
Staa huyo raia wa Kenya, mwaka jana alifanikiwa kuchukua tuzo ya BET nchini Marekani pamoja na tuzo ya Oscar kupitia filamu ya ‘12 years a Slave’.
Lupita amesema kwenye filamu hiyo mpya watu watapata shida kumtambua mapema, lakini watamuelewa mwishoni, hasa kutokana na mwonekano wa mavazi yake.
“Natarajia kuonekana tena Desemba hii kwenye filamu ya Star Wars ambayo ni ‘episode’ ya saba, ni filamu ya kusisimua, watu wakae tayari kuipokea kazi hiyo,” alieleza Lupita.