25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Kikwete atunukiwa tuzo ya demokrasia

Jakaya Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete

RAIS Jakaya Kikwete ametunukiwa tuzo ya kimataifa ya Nyota wa Demokrasia Afrika 2014.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana, Rais Kikwete aliandikiwa barua ya kuwa mshindi wa kwanza katika mchuano huo uliohusisha marais watatu wa Afrika ambao waliingia katika tatu bora.

“Katika barua hiyo, Mchapishaji na Mhariri Mkuu wa Jarida hilo, Pastor Elvis Iruh, akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Tuzo 2014, amesema kuwa uongozi wa Rais Kikwete umekuwa ni hadithi ya kusifiwa ya mafanikio katika Bara ambako hadithi za namna hiyo siyo nyingi,” ilieleza taarifa hiyo ya Ikulu

Tuzo hiyo hutolewa na Jarida la The Voice ambapo mwaka jana mshindi alikuwa Rais Bai Koroma wa Sierra Leone, ambayo ilitolewa kwa mara ya kwanza kwa Rais wa Kwanza wa Zambia, Kenneth Kaunda.

Sherehe maalumu ya kukabidhi tuzo hiyo imepangwa kufanyika Oktoba 17, mwaka huu, katika Hoteli ya Van der Valk, iliyoko Almere, nchini Uholanzi.

Taarifa hiyo imeeleza miongoni mwa sifa nyingine Rais Kikwete alizotunukiwa tuzo hiyo ni msimamizi mzuri na wa kweli wa demokrasia, kuendelea kuhakikisha kuwa amani, utulivu na maendeleo vinaendelea kupatikana katika eneo la Afrika ambalo limepitia vipindi vingi vya migogoro na matatizo.

“Gazeti hilo linasema kuwa Rais Kikwete amekuwa kiongozi wa mfano, kimataifa na kikanda na linatoa mfano wa mchango wake katika kusuluhisha mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini Kenya, kufuatia uchaguzi mkuu wa 2007.

“Rais Kikwete pia anasifiwa kwa mchango wake katika kusimamia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali – kilimo, elimu, miundombinu, maendeleo ya viwanda, utalii na pia mchango wake katika kuendeleza vijana na kutoa nafasi nyingi kwa akinamama kushika nafasi nyingi za uongozi,” ilieleza taarifa hiyo.

Aprili mwaka huu, Rais Kikwete alitunukiwa tuzo ya kuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya Afrika kwa mwaka 2013 – The Most Impactful Leader in Africa 2013.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles