23 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Ukawa wamgomea Samuel Sitta

Samuel Sitta
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta

Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

WAJUMBE wa Kamati ya Mashauriano ya Bunge Maalumu la Katiba wamekutana jana kwa ajili ya kujadili hatima ya Bunge hilo linalotarajiwa kukutana Agosti 5, mwaka huu.

Kamati hiyo imekutana bila ya kuwepo kwa wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao pia ni wajumbe wa kamati hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alisema kuwa taarifa kamili za maazimio ya kikao hicho zitatolewa leo.

“Jana tulipanga kuwaeleza wananchi yaliyojiri kwenye kikao hicho, kutokana na muda kuchelewa, tutatoa taarifa hizo kesho (leo) saa tatu asubuhi,” alisema Sitta.

Vyanzo vya habari kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo vilidai kuwa kamati hiyo imeazimia kuendelea na vikao vya Bunge hilo kama kawaida, hata kama wajumbe wa Ukawa hawatashiriki.

“Tulichoamua ndani ya kikao ni kuendelea na vikao vya Bunge Maalumu la Katiba kama kawaida, hata kama wajumbe wa Ukawa hawatashiriki kwenye kikao hicho,” kilisema chanzo hicho.

Kilidai kuwa, siku ya kikao cha kwanza mwenyekiti na makamu wake watahesabu akidi kama imetimia ili waweze kuendelea na kikao hicho kama kawaida.

Alisema, wajumbe wasioshiriki kwenye kikao hicho hawaitakii mema nchi yao, kwa sababu wanataka kuvuruga mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.

“Ikiwa akidi itatimia, wajumbe wataendelea na kikao kama kawaida, lakini pia tutawaambia wananchi kuwa wajumbe wasioshiriki hawaitakii mema nchi yao,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, wajumbe wa Ukawa ndio waliodai kutoshiriki kwenye vikao vya Bunge Maalumu la Katiba kwa madai mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wajumbe wenzao, wakiwamo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujadili mambo yasiyokuwamo ndani ya rasimu ya katiba.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. CCM achenikuendelea kuhadaa watanzania, ninyi ndiyo mnaovuruga mchakato siyo Ukawa. Hat mkisema ati mtawaambia wananchi wasioshiriki vikao vya bunge la katiba yaani Ukawa ndiyo wasioitakia nchi mema, mnapoteza muda bure, kwani wananchi wote kwa sasa wanajua ni wajumbe CCm na viongozi wao akiwamo Rais ambao hawataki katiba mpya. Mbona mnawafanya watanzania kama ni wapumbavu hawajui nani kalikoroga? Chakufanya kama kuna busata imepbaki, ni CCM kuwa wanyenyekevu na kusema, imeshindikana, basi tusitishe mchakato tuokoe pesa za wananchi mchakato uhairishwe, kwa kweli hapo wananchi watawaona ni wa tu wa busara. Kuendelea kujidai mnajua kuliko wengine ni kuendelea kulifanya bunge la katiba ligeuke kuwa kaburi Rasmi la CCM. kama hili hamlijui, basi habari ndiyo hiyo, CCM jifunzeni kusoma alama za Nyakati, kipenga kimelia, wananchi wamchoka na porojo zenu. “Asiyesikia la mkuu atavunjika guu.” Mwenye masikio na asikie, Watanzania siyo wajinga, sasa wameamka sana, wala msijidanganye kwa hilo itakula kwenu. Busara iliyobaki ni kusitisha bunge la katiba la sivyo kura ya maoni itakuwa ni anguko kubwa la serikali ya CCM na kishindio chake kitasikika dunia nzima. Tunaosema ukweli mtanatuona kwamba tuna chuki na CCM lakini mtatukumbuka yatakapotokea yakutokea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles