30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisi za MSD zateketea kwa moto

moto
Meneja wa Bohari ya Madawa Kanda ya Tanga (MSD), Mwanasheha Jumaa, akiwaonyesha mafundi baadhi ya maeneo yaliyoungua kwa moto kwenye ofisi hiyo ya watumishi kutokana na hitilafu ya umeme na kuteketeza vitu vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 20 jana. Picha na Oscar Assenga.

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

OFISI ya Watumishi katika Bohari ya Madawa Kanda ya Tanga (MSD) imeteketea kwa moto baada ya kutokea hitilafu ya umeme jana saa kumi alfajiri na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh milioni 20.

Akithibitisha kutokea kwa moto huo jana, Meneja wa MSD Kanda ya Tanga, Mwanasheha Jumaa, alisema tukio hilo limewashtua, hasa tangu alipopata taarifa za moto huo kutoka kwa walinzi.

Mwanasheha alisema baada ya walinzi hao kufahamu tukio hilo walijitahidi kuanza kuuzima moto huo ambao ulikuwa ukiendelea kusambaa kwenye baadhi ya maeneo kwenye ofisi hiyo na kufanikiwa kuuzima.

Alivitaja vitu vilivyoungua kwenye ofisi hiyo kuwa ni mifumo ya mawasiliano ya intaneti, vipoza joto na samani za ofisi.

Alisema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.

“Tukio hili limetusikitisha sana na kutuacha hatuna kitu kwenye ofisi hii ya watumishi, kama unavyoona hivyo sasa tunajipanga kuhakikisha jambo hili halijitokezi tena,” alisema Mwanasheha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles