25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi walia KCMC kukosa CT Scan

Hospitali ya KCM Moshi
Hospitali ya KCM Moshi

Na Rodrick Mushi, Moshi

WANANCHI wa Mkoa wa Kilimanjaro wamelalamikia hatua ya uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC kushindwa kutoa huduma ya CT Scan tangu mashine hiyo ilipoharibika mwaka 2012, hali inayosababisha adha.

Wakizungumza na MTANZANIA jana mjini Moshi, wamesema tangu mashine ya CT Scan ilipoharibika, wanalazimika kusafiri kwenda jijini Arusha kufuata huduma hiyo kwa gharama ya Sh 300,000.

Akizungumza kwenye maeneo ya Hospitali ya KCMC, Amon Mmari alisema awali wagonjwa walikuwa wakipatiwa huduma hiyo kwa Sh 80,000 hadi 150,000, lakini tangu ilipoharibika vifo vingi vimekuwa vikiripotiwa, hali iliyochangiwa na kukosekana kwa huduma hiyo.

Hospitali ya Rufaa ya KCMC inahudumia zaidi ya wananchi 35,000 kwa siku kutoka ndani na nje ya nchi.

Awali akizungumza na gazeti hili, Kaimu Mkurugenzi wa KCMC, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma wa Hospitali ya KCMC, Profesa Raimos Olomi, alikiri kuwa tangu mashine ya CT Scan ilipoharibika mwaka 2012 hospitali hiyo haitoi huduma hiyo.

Alisema mashine hiyo ilipoharibika hospitali hiyo ilijaribu kuifanyia marekebisho, lakini ilishindikana ambapo kwa sasa mashine mpya inagharimu hadi Sh bilion 1.6.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles