23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wanane wahofi wa kufukiwa machimbo ya dhahabu Kahama

kamugishaNA PAUL KAYANDA, KAHAMA

WATU zaidi ya wanane wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo katika machimbo ya Nyangarata katika Kata ya Lunguya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema tukio hilo lilitokea juzi asubuhi baada ya watu wapatao 20 kuingia katika shimo la uchimbaji dhahabu na kifusi hicho kikaanguka wakiwa ndani.

Alisema ingawa idadi kamili juu ya waliokuwa ndani ya shimo inakadiriwa kuwa 20 lakini baada ya ufuatiliaji wa kina inakadiriwa iwapo kuna watu watakuwa walibakia ndani ya shimo hilo idadi yao inaweza kuwa wanane ingawa
wachimbaji hao wanadai wanaweza kuwa 11.

Kamanda alisema jitihada za serikali kuhakiki na kufuatilia watu ambao wanaweza kuwa wamefukiwa ndani ya shimu hilo zinaendelea kufanyika kwa kuwa baadhi ya wanaotajwa kufukiwa simu zao zimekuwa zikiita hali inayoonyesha kuwamo kwao shimoni.

Diwani aliyemaliza muda wake katika Kata ya Lunguya, Benedict Manwari alisema mpaka sasa idadi ya watu waliookolewa baada ya kuangukiwa na shimo hilo ni 11 ambao wamejeruhiwa sehemu na kukimbizwa kwenye Kituo cha Afya cha Luguya kwa matibabu.

Alisema kwa sasa wanaendelea na jitihada za kuokoa wachimbaji wengine ambao inasadikika bado wamo ndani ya mashimo kwa kushirikina na kikosi cha uokoaji kutoka katika Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu.

Naye Ofisa Madini Mkazi wa Wilaya ya Kahama, Sophia Omary alisema amelazimika kusafiri kwenda eneo la tukio kuangalia machimbo hayo na jinsi uokoaji unavyofanyika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles