27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

KiliFest 2015 ilivyofana Dar

mtz31NA TUNU NASORO

UMAHIRI ulioonyeshwa na wasanii waliotumbuiza katika Tamasha jipya la KiliFest lililofanyika kwa mara ya kwanza katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam umeonyesha dira na mwelekeo wa tamasha kubwa zaidi kwa
mwakani.

Tamasha hilo lililodumu takribani saa 18 baada ya kuanza saa nne asubuhi na kumalizika saa tisa na nusu alfajiri lilipokelewa kwa shahuku kubwa na Watanzania wapenda burudani ambao wengi wao walipongeza nia ya tamasha
hilo, ikiwemo kulipeleka mikoa mingi zaidi kwa mwaka ujao.

Majira ya saa 11 jioni tamasha lilianza ambapo burudani kali kutoka kwambwembwe nyingi jukwaani, Isha Mashauzi, zilianza huku shamra shamra za mashabiki zikirindima kwa shangwe.

Baada ya Isha Mashauzi, wasanii wengine walioacha gumzo katika tamasha hilo kwa kufanya shoo ya nzuri ni bendi ya Mapacha Watatu, Maua, Ruby, Damian Soul, Navy Kenzo, Fid Q, Ben Paul, Vanessa Mdee, Shettah na kundi la Weusi lililoshangiliwa kila lilipotamka neno lililopo katika wimbo wao.

Mashabiki walionyesha kufuatilia kila kilichoimbwa kwa kufuatia kila neno la lililoimbwa katika nyimbo za wasanii hao, huku wakiongeza vionjo kwa kucheza kwa ustadi wa hali ya juu pamoja na wasanii wa kundi hilo kiasi kwamba kila aliyefika katika tamasha hilo alinogewa.

“Tulidhamiria kufanya kitu kizuri na kimefanyika hivyo wapenzi wa burudani wamelipokea na wametupa mwanga wa kuwaandalia vitu vizuri zaidi kwa tamasha lijalo la mwakani,’’ Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli anasema.

Kikuli anaongeza kwamba maandalizi ya tamasha hilo waliyafanya kwa muda mrefu kiasi kwamba walihakikisha kila
anayeshiriki anapata anachotarajia katika tamasha hilo lililokuwa likishereheshwa ikwa vionjo kutoka kwa MaDJ, DJ Summer, DJ Zero na DJ Mafuvu.

Katika kujali zaidi mashabiki wake waandaaji wa tamasha hilo walijipanga katika mazingira yote kwa kuweka runinga kubwa zilizowawezesha waliohudhuria kushuhudia mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, ambapo
matokeo yalikuwa Yanga 2 Simba 0.

Michezo mingine iliyokuwa ikivutia wengi ni kuimba kwa kutumia kifaa maalumu (kilioke), mpira wa mezani (fuse ball) ambapo wengi walishinda na wakapatiwa zawadi mbalimbali zilizoongeza chachu ya kunogesha tamasha hilo
ambalo pia lilikuwa na viburudisho mbalimbali, ikiwemo vyakula vya kila aina na muziki na vinywaji
mbalimbali, ikiwemo bia za Kilimanjaro.

Kutimiza ahadi yao waandaaji walifanya kila lililowezekana kwa washindi waliopatikana katika michezo mbalimbali
wakajumuishwa katika mazungumzo na mastaa waliokuwepo katika tamasha hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles