26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ajali ya gari yaua watu watano

Ramadhani Mungi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi

NA RAYMOND MINJA, IRINGA

WATU watano wamefariki dunia mkoani Iringa, baada ya lori la mizigo lililokuwa likielekea mkoani Mbeya kuacha njia na kugonga nyumba.

Lori hilo liliparamia nyumba hiyo ambayo ilikuwa ni kilabu cha pombe za kienyeji katika Kijiji cha Ugwachanya na kuua watu watano papo hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 4 usiku katika Kitongoji cha Isimila.

Kamanda Mungi alisema ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T 570 AYT aina ya Mercedes-Benz, mali ya Mt Huwel ya mjini Iringa lililokuwa likiendeshwa na dereva, Juma Omary (40), mkazi wa Makorongoni mjini hapa.

Mungi alisema wakati ajali hiyo ikitokea, watu hao walikuwa wakiendelea kunywa pombe katika kilabu hicho na ghafla walijikuta wakifuatwa na lori hilo, ambalo lilikuwa limeacha njia na hatimaye kusabaratisha kilabu hicho.

Marehemu waliotajwa kupoteza uhai katika ajali hiyo, ni Leonard Mkendela (35), Neema Mkendela na Kamsia Mkendela wote wa familai moja na Ester Mwalomo pamoja na Oscar Zosama (25), ambao ni mume na mke.

Kamanda Mungi aliwataja majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni Juma Abdallah, Omary Ally (40), ambaye alikuwa akiendesha gari hilo, Kasimu Mambo (44), pamoja na Mussa Abdallah Kadege (34), ambao wote ni wakazi wa Kijiweni mjini Iringa.

Alisema majeruhi wote wamelazwa katika Hopitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles