24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mitt Romney ; Gavana wa Marekani aliyetoa hotuba darasa kwa magufuli na Lowassa.

mitt romneyNa Michael Maurus kwa msaada wa mitandao

GAVANA wa 70 wa Marekani, Mitt Romney, aliwahi kutoa hotuba ya aina yake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mwaka 2012, ambayo hadi leo imebaki kuwa darasa tosha kwa wanaojitokeza kuwania uongozi.

Kwa hapa Tanzania, hotuba hiyo inaweza ikawa somo kwa wale wote waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kama John Maguli, Edward Lowassa, Anna Mghwira na wengineo wanaowania urais.

Wakati Magufuli akiwania nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lowassa anawakilisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), huku Anna akijitupa katika kinyang’anyiro hicho kwa tiketi ya ACT- Wazalendo.

Lakini pia, hotuba hiyo ya Romney, inawalenga wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliopangwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu. Wiki iliyopita tuliona jinsi Romney alivyowahamasisha Wamarekani kutofanya kosa katika uchaguzi kwani tukio hilo lina maana kubwa kwa majaliwa ya nchi yao hiyo na familia zao kwa ujumla.

Alisema wapiga kura ni vyema wakawapima kwa kina wagombea kwa kuchuja sera zao na kutafakari iwapo wana uwezo wa kuyatekeleza kwa dhati yale wanayohubiri majukwaani. Aliwapasha Wamarekani kutokubali kurubuniwa, wakifahamu kuwa kosa lolote wanaloweza kulifanya katika uchaguzi huo, linaweza kulipeleka pabaya Taifa lao na kuzisambaratisha familia zao.

Endelea kupata ujumbe wa nguvu kutoka kwa Romney ambao si tu unawapa somo wapiga kura, lakini pia unawaelekeza wagombea kuona ni mambo gani ya msingi wanatakiwa kuyazingatia ili waweze kufanikiwa katika mchakato wa uchaguzi.

Endelea… Uchaguzi huu ndio utakaotoa mwanga kwa wataalamu wote wa nyanja mbalimbali kuona ni vipi wanaweza kunufaika na taaluma zao. Hapa namaanisha madaktari, askari, walimu, waandishi wa habari, wanamichezo na wasanii na wanataaluma wengineo.

Lakini pia uchaguzi huu ndio utakaotoa nafuu kwa wagonjwa ambao wanapokwenda kuwaona madaktari, huambiwa na mtu wa mapokezi kuwa daktari hahitaji mgonjwa mwingine, kwa kuwa hakuna dawa. Uchaguzi huu ndio utakaoamua maisha yetu yaweje, aidha tuishi kwa dhiki au tuwe na maisha mazuri, tena kwa usawa miongoni mwa raia wote wa Marekani.

Una maana kubwa kwa wanafunzi, wanavyuo ambao wamekuwa wakihaha kupewa mikopo ya masomo yao, hali inayohatarisha kutimiza majaaliwa yao ya kutimiza ndoto zao katika elimu. Una maana kubwa kwa watoto wanaoshindwa kwenda shule, ambao hawawezi kwenda kwenye shule wanazopenda wazazi wao.

Kaulimbiu ya kampeni za Rais aliyepita ilikuwa ni ‘mbele kwa mbele’. Lakini milioni 23 ya Wamarekani wamekuwa wakihaha kutafuta kazi bila mafanikio. Na kwa hali ilivyo, badala ya mbele kwa mbele, sasa inaonekana wazi tunazidi kurudi nyuma na hatuwezi kuhimili hata miaka minne ijayo.

Uchaguzi huu una matokeo makubwa muhimu, kwanza juu ya elimu ya watoto wetu, thamani ya makazi yetu, mishahara tunayolipwa makazini kwetu, bei za bidhaa tunazonunua na juu ya suala zima la huduma za afya. Lakini pia uchaguzi huu una maana kubwa katika ukuaji wa uchumi wetu, nguvu ya majeshi yetu, utegemezi wetu katika mafuta kutoka nje na utawala wa Marekani katika dunia ya leo.

Mara kadhaa Rais Barrack Obama alikuwa akitukumbusha kuwa alirithi hali ngumu ya kiuchumi. Lakini hilo si tu ambalo Rais Obama alilirithi. Alirithi Taifa kubwa katika historia ya Dunia hii. Alirithi Taifa linalozalisha zaidi na lenye ubunifu wa hali ya juu katika historia ya ulimwengu huu. Alirithi Taifa lenye nguvu kubwa kiuchumi.

Na pia alirithi watu ambao wamekuwa na msisimko wa hali ya juu katika tukio lolote, bila kujali changamoto lukuki zinazowakabili, kwa kuwa tumeongozwa na wanaume na wanawake ambao wamekuwa pamoja kwa muda mrefu. Pamoja na kurithi yote hayo, Rais Obama hakuweza kuukarabati uchumi wetu, hajasaidia kuimarisha huduma ya afya na ulinzi wa kijamii au kupambana na China ambayo imekuwa ikizidi kujitanua kiuchumi katika kila kona ya dunia.

Kwa hali ilivyo sasa, mambo yanaonekana kuwa magumu zaidi ya alivyoikuta nchi. Familia nyingi zimeshindwa kupata huduma za msingi na wajasiriamali wengi wameshindwa kupata mikopo kutokana na sheria ngumu zinazowabana kuweza kukopeshwa na mabenki.

Kumetumika fedha nyingi kwa ajili ya uwekezaji ambao mwisho wa siku, umewanufaisha wachache na kuiingizia deni Serikali. Bei ya nishati imezidi kupanda kwa sababu uzalishaji umeshuka. Ni kutokana na hali hiyo, maisha yetu yamezidi kuwa mabaya, kinamama wakizidi kuwa masikini.

Leo tumekuwa tukipata habari mbaya zaidi zinazozidi kutukatisha tamaa juu ya uchumi wetu. Kukua kwa kasi ndogo kwa uchumi kunamaanisha kuzidi kuporomoka kwa nafasi za kazi na kupungua kwa mishahara. Wamarekani kwa sasa wapo tayari kwa mabadiliko ambayo yatasaidia kukua kwa uchumi, kuongezeka kwa nafasi za kazi pamoja na mishahara.

Usikose toleo lijalo la MTANZANIA Jumatano uweze kuona jinsi Gavana Mitt Romney alivyotoa darasa la nguvu
kwa Wamarekani kuelekea uchaguzi wa nchi hiyo, ambalo linaweza kuwa dira ya Watanzania wanaojiandaa kushiriki uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles