23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Magufuli: Kama kungekuwa na mashindano ya ilani, CCM ingeshinda

ccmNa Bakari Kimwanga

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema kama kungekuwa na mashindao ya ilani bora ya uchaguzi, chama chake kingeongoza kwani kina ilani nzuri kuliko vyama vingine.

Alisema vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), havina ilani inayoweza kutatua matatizo ya Watanzani hivyo ni vyema wananchi wasihadaike nao.

Ukawa inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, walizindua kampeni na ilani yao juzi jijini Dar es Salaam na kuweka vipaumbele vyao ikiwamo kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya chekechea mpaka chuo kikuu na kila mwananchi kupata tiba bora na nafuu.

Jana Dk. Magufuli akihutubia wananchi kwenye mikutano iliyofanyika katika wilaya za Ludewa na Songea, alisema ilani ni mkataba kati ya wananchi na chama kinachoomba ridhaa lakini hilo limekuwa tofauti kwa vyama vya Ukawa.

“Sijui kuna vyama vitano vimeungana na kuwa na ilani moja ya uchaguzi, hapo hakuna kitu, chama chenye mgombea ndicho kinakuwa na ilani.

“Ilani ni mkataba kati ya wananchi na chama kinachoomba ridhaa, sasa Ukawa ni muungano wa vyama, ilitakiwa kila chama kiwe na ilani yake, Ukawa hawana ilani ila CCM ndiyo imejipanga kuomba ridhaa na ina ilani bora na yenye kutekelezeka kwa uhakika,” alisema Dk. Magufuli.

Kutokana na hali hiyo, alisema anaomba urais si kwa ajili ya kufanya majaribio ila anataka kuwatumikia Watanzania kwa vitendo.

“Ninapenda kuwaambia leo nipo hapa Ludewa lakini mbunge wenu ni mbunge mkweli na mfuatiliaji wa mambo.

“Baada ya uchaguzi tunaanza kuitengeneza hii barabara kutoka Njombe hadi Ludewa ili kuchochea na kuimarisha uchumi, Filikunjombe pamoja na wananchi ni lazima niwape zawadi ya lami.

“Ludewa ina mradi mkubwa wa makaa ya mawe, ni lazima tufungue njia… ninajua hapa kuna tatizo la maji nitashughulikia kwa wakati,” alisema Dk. Magufuli.

 

Filikunjombe na kilio

 

Awali akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Mlangali, Mbunge mteule wa Ludewa, Deo Filikunjombe, alisema anatambua utendaji kazi wa Dk. Magufuli.

Alisema pamoja na hali hiyo, lakini bado kuna changamoto kadhaa ikiwemo tatizo la maji safi na salama katika kata hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles