27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mshindi wa TMT kupokelewa Arusha leo

DENNIS-294x300YULE msanii wa maigizo chipukizi aliyeshinda milioni 50 katika shindano la Tanzania Movie Talent (TMT), Denis Lwasai, anatarajiwa kuwasili jijini Arusha leo akitokea jijini Dar es Salaam ambako shindano hilo lilifanyika.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili, mshindi huyo anatarajiwa kuanzia msafara wake kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA asubuhi ambapo watu mbalimbali wameombwa kufika kwa ajili ya kumpongeza mshindi huyo pamoja na kupiga naye picha za kumbukumbu.

Mshindi huyo aliyewahi kufanyakazi na marehemu Steven Kanumba, aliibuka na kitita hicho na kuwashinda wenzake 10 walioingia katika fainali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles