27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm agomea mechi Yanga

JO6A1062NA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, raia wa Uholanzi, amegoma kucheza mechi za kirafiki kwa ajili ya kujipima nguvu hadi nyota wake watakaporejea kutoka kwenye timu zao za Taifa ambazo wamekwenda kuzichezea.

Kocha huyo, ambaye hajafungwa mechi hata moja ya kirafiki, inawezekana hataki kuivuruga rekodi hiyo kutokana na kuwakosa nyota hao, ambao wamekuwa chachu ya ushindi kwenye kikosi hicho ambacho kilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania msimu uliopita.

Nyota wa Yanga walioungana na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kilichoondoka kwenda Uturuki ni kipa Ali Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Deus Kaseke, Salum Telela na Simon Msuva.

Wachezaji wa kulipwa ambao wameitwa kwenye vikosi vya timu zao za taifa ni kiungo mchezeshaji Haruna Niyonzima na washambuliaji Amissi Tambwe na Donald Ngoma.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alisema ni lazima wawasubiri wachezaji hao ambao ni muhimu kwenye kikosi, huku akidai kama itawezekana wanaweza kucheza mechi za kirafiki na timu za hapa nyumbani.

Yanga walipata nafasi ya kujipima mechi za kimataifa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) na kucheza mechi kadhaa za kirafiki walipoweka kambi Tukuyu, Mbeya ambako walifanikiwa kushinda dhidi ya Mbeya City, Tanzania Prisons na Kimondo FC.

“Kwa sasa tunasubiri kwanza hadi wachezaji wote watakaporudi baada ya kuzichezea timu zao za taifa kwenye mechi za kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Gabon, lakini ikiwezekana tutaweza kucheza,” alisema.

Mechi za timu za taifa kwa mujibu wa CAF zimepangwa kufanyika kati ya Septemba 5 na 7, mwaka huu, ambapo Stars, yenye wachezaji wanane wa Yanga, itaumana na Nigeria ‘Super Eagles’ Septemba 5, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles