27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yawatuliza nyota wake

NA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wamepanga kuwatuliza nyota wao kwa kuanzisha mipango endelevu ndani ya klabu hiyo ambayo itawahamasisha na kuwavutia kuendelea kuitumikia timu yao kwa mafanikio msimu ujao.
Kwa sasa Yanga inajiandaa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) itakayofanyika Julai, mwaka huu nchini.
Lakini baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Mei 9 mwaka huu, Yanga wameendelea kuvuta subira kwenye usajili wakisubiri maamuzi ya ripoti ya kocha wao mkuu Mholanzi, Hans van der Pluijm, ambaye yupo mapumzikoni.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Jonas Tiboroha, alisema jana kuwa hakuna mchezaji anayependa kusajiliwa na timu isiyokuwa na mikakati endelevu ya ushindi, hivyo jitihada zao ni kuhakikisha wanawabakiza nyota wao muhimu kwa uhakika wa mafanikio ya baadaye.
Kauli ya Tiboroha imetokana na usumbufu wanaopata kutoka kwa nyota wa kulipwa wa klabu hiyo, kiungo Haruna Niyonzima na beki Mbuyu Twite, ambao wanadaiwa kugoma kusaini mikataba ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi sasa.
“Hayo ni mambo ya kawaida kwa wachezaji, hasa wa kulipwa kufuatilia mipango ya timu wanazokwenda kwa kutaka kujua mikakati waliyojiwekea katika kukabiliana na ushindani kwenye michuano mbalimbali,” alisema.
Niyonzima na Twite waliondoka nchini na kwenda kwao mapunzikoni baada ya ligi kumalizika, huku wakiwa bado hawajamalizana na Yanga, ambao wanawasubiri watakaporejea ili waweze kukamilisha taratibu za usajili wao kwa msimu ujao na michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwakani.
Nyota hao wanaotajwa kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa, ni miongoni mwa wachezaji wa kulipwa wanaotakiwa kubaki ndani ya kikosi hicho kutokana na viwango vyao kukubalika na Pluijm.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles