24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Madabida augua ghafla sherehe za Mei Mosi

Ramadhani-MadabidaRuth Mnkeni, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida jana aliugua ghafla wakati akiwa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru ulioko Wilaya ya Temeke.
Madabida ambaye haikufahamika mara moja aliugua nini, alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Gazeti hili ambalo lilikuwa uwanjani hapo jana, lilimshuhudia Madabida akisaidiwa na baadhi ya watu waliokuwa karibu naye baada ya kuzidiwa muda mfupi baada ya kuhitimishwa kwa maadhimisho hayo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alikuwa mgeni rasmi.
Baadhi ya viongozi wa chama na Serikali waliokuwapo uwanjani hapo walimzunguka baada ya kukumbwa na hali hiyo kisha walimpandisha ndani ya gari maalumu la kubebea wagonjwa (Ambulance) la Muhimbili lenye namba STK 7374 aina ya IVECO ambalo liliondoka kwa kasi uwanjani hapo kuelekea Muhimbili.
Hata hivyo, haikuweza kujulikana mara moja tatizo lililomkumba Madabida na kumsababishia hali hiyo.
Awali akizungumza na wafanyakazi waliohudhuria maadhimisho hayo, Sadick aliwataka kuvuta subira kwa kuwa Serikali inashughulikia suala la mishahara yao.
“Naomba mvute subira kuhusu mishahara, Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma inalifanyia kazi suala hili pamoja na Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira.
“Katika Bunge litakalofanya kikao chake mwanzoni mwa mwezi huu, taarifa ya Serikali itatolewa na taasisi na mawaziri wenye dhamana na Wizara hizi mbili,” alisema.
Sadick alisema jumla ya walimu 4,212 wamelipwa stahili zao ambapo 3,390 ni wa shule za msingi na 822 wa shule za sekondari.
“Aidha, kiasi cha Sh bilioni 1.5 kimelipwa kwa walimu 3,646 ambapo 2,664 ni walimu wa shule za msingi na 982 wa sekondari kwa ajili ya likizo na stahili zao wakiwa masomoni na malipo ya wastaafu,” alisema Sadick.
Sadick aliwapongeza viongozi wa Manispaa kwa jitihada walizozifanya katika kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la ujenzi wa maabara ndani ya mkoa huo.
Alisema hadi kufikia Aprili 10, mwaka huu jumla ya majengo ya maabara mpya 281 yamekwishajengwa.
“Ilala zimejengwa maabara 76, Kinondoni 126 na Temeke 79 ambapo uwiano unaonyesha zimekamilika kwa asilimia 100 na 27 kati yake zimeshaanza kukamilika na ukamilishwaji wa uwekaji wa mifumo ya gesi na maji kwa maabara 254 unaendelea,” alisema Sadick.
Alisema hata hivyo bado mkoa huo unakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 42,434 kwa shule za msingi, matundu ya vyoo 14,406 na madarasa 467 kwa shule za sekondari na matundu ya vyoo 33,502.000222222222222222

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles