27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TUCTA yadai nyongeza ya mishahara

nmgayaNa John Maduhu, Mwanza

SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limeitaka Serikali kuhakikisha inaongeza kima cha chini cha mshahara ili kuwawezesha wafanyakazi kujikimu kimaisha.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Nicolaus Mgaya, wakati akisoma risala ya wafanyakazi mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani, iliyofanyika kitaifa katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Mgaya alisema Serikali inapashwa iongeze kima cha chini ya mshahara hadi kufikia shilingi 310,000/ kwa mwezi kwa wafanyakazi wa Serikali na kwa sekta binafsi sh 120,000.

Alisema katika sekta binafsi hali ya mishahara inayolipwa haikidhi mahitaji ya wafanyakazi kwa kuwa baadhi ya waajili ni wakorofi na hadi sasa wanalipa sh 60 kwa mwezi.

Wailipua CMA
Mgaya aliituhumu Tume ya Usuluhishi wa Migogoro sehemu za kazi (CMA) kuwa inajihusisha na vitendo vya rushwa na inachelesha utoaji wa hukumu kwa mashauri mbalimbali.
Alisema awali CMA ilianza kazi vizuri kwa kutatua kwa kasi kero mbalimbali ilizokuwa ikifikishwa lakini katika siku za hivi karibuni imeonekana kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

“Awali CMA walikuwa wakitumia muda wa siku 30 kutatua migogoro lakini sasa inachukua hata mwaka mmoja kutoa uamuzi wa kesi, pia kuna vitendo vya rushwa, tunaomba uchunguzi ufanyike,” alisema.
TAMISEMI
TUCTA pia imeitaka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), kuhakikisha inakabiliana na tatizo la uhaba wa watumishi katika halmashauri hapa nchini.

Alisema badhi ya halmashauri zimekuwa zikikabiliwa na tatizo la wataaalamu katika sekta za mipango miji na maafisa ardhi, hali inayosababisha usumbufu kwa wananchi kupata huduma.
ULINZI WAIMARISHWA
Hali ya ulinzi katika uwanja wa CCM Kirumba jana ilikuwa imeimarishwa huku kila mwananchi aliyekuwa akiingia katika uwanja huo akikaguliwa kwa vifaa maalumu na vikosi vya ulinzi na usalama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles