23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Clouds Media yang’ara tuzo za ubora

rugeNa Adam Mkwepu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kung’ara katika tuzo za ubora na viwango vya bidhaa (superbrands) baada ya majumuisho na uchambuzi wa kina kufanyika.
Tuzo hiyo ya mwaka 2015-16 ilitolewa na Taasisi ya Uchambazi wa Viwango yenye makao makuu London Uingereza.
Utoaji wake kwa kampuni zinazohusikana kutoa huduma na kuzalisha bidhaa umeelezwa unazingatia ushauri wa wataalamu wa masoko na maoni ya watumiaji zaidi ya 600.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya utoaji wa tuzo uliofanyika Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alisema mafanikio hayo yanatokana na kushirikiana na jamii katika kutoa elimu na burudani.
“Awali tulianza kama radio ya burudani pekee na tumebadilika baada ya kugundua kuwa tuna wajibu wa kutoa huduma kwa watu wengine, ikiwa ni kuthibitisha uzalendo wetu kwa jamii na hivi sasa kituo chetu ni sehemu ya elimu na burudani kwa wote,” alisema Mutahaba.
Alisema licha ya kuzawadiwa mara ya pili tuzo hiyo kwa upande wa radio, pia kituo kinaahidi huduma bora kwa jamii na yenye viwango katika kila idara ndani ya kampuni hiyo lengo likiwa ni kuifikia Afrika kwa ujumla.
Mkuu wa Taasisi hiyo Afrika Mashariki, Jawad Jaffer alisema katika utoaji wa tuzo hizo yamezingatiwa maoni ya wataalam wenye uzoefu wa masoko na walengwa wa huduma na bidhaa ambao wana haki ya kuamua aina ya viwango bora vya superbrands.
“Nawapongeza kwa kuwa miongoni mwa makampuni ambayo yamebakia katika orodha ya 20 bora ambako Clouds FM imefanikiwa kuwa katika mafasi ya nane huku ITV ikiwa nafasi ya nne,” alisema Jaffer.
Alisema kampuni 11 zinazotoa huduma za kuzalisha bidhaa zimeendelea kung’ang’ania kwenye orodha ya 20 bora ya superbrands.
Alizitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni Chai bora, Kilimanjaro Awards, Foma Gold, Kilimanjaro Premium Lager, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mlimani Shopping Center, Safari Lager na Precision Air.
“Zaidi ya kampuni 1000 nchini zilipambanishwa zikafanyiwa upembuzi na utafiti wa kina jambo linalofanya taasisi zilizoingia kwenye 20 bora kufurahia nafasi zao kutokana na utendaji na mafanikio kama ilivyofafanuliwa na wataalamu wa masoko na maoni ya wateja, ”alisema Jeffer.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles