27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

NHC yaongeza miradi ya bilioni 600/=

Nahemiah MchechuNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, amesema shirika hilo limefanikiwa kuongeza miradi yake na kufikia Sh bilioni 600 kwa miaka mitano.
Mafanikio hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wahariri, aliwaambia kwamba mafanikio hayo ni mwanzo na wanatarajia kupata zaidi katika miaka miwili ijayo.
“Mwaka 2010 shirika hili lilikuwa na miradi ya Sh bilioni 4 lakini hivi sasa tumefanikiwa kufikisha bilioni 600 na natarajia miaka miwili ijayo tutaongeza miradi zaidi ya hapo na kufikia trilioni kadhaa,” alisema.
Akielezea mafanikio mengine waliyopata mkurugenzi huyo alisema kuwa kwa sasa wamefanikiwa kuwa na miradi katika mikoa mingi na wanajipanga kupeleka miradi ya nyumba kila wilaya.
“Wito wangu umebaki kwa wateja wa kada mbalimbali kujitokeza kununua nyumba zetu ambazo kwa miaka saba ijayo tutakuwa tumefika kila wilaya ikiwamo na mipakani mwa nchi,” alisema.
Mchechu alikiri kutofanikisha mkakati wao wa kujenga nyumba 15,000 katika mwaka huu ingawa alisema hadi kumalizika kwa mwaka huu watakuwa wamekaribia kuzifikia.
“Ujenzi huo wa nyumba15,000 ambao tulipanga kujenga nyumba 3,000 kwa mwaka ambazo hadi sasa tumefikisha nyumba 7,000. Naamini hatutamaliza zote kwa mwaka huu ila tutasogea,” alisema.
Mkurugenzi huyo wa NHC alifafanua kuwa kuchelewa kwa ujenzi huo kumechangiwa kwa muda wa miaka miwili alizotumia kufanya mageuzi ya nyumba huku miaka mitatu wakiitumia kuzijenga.
Kuhusu suala la msamaha wa kodi kwa nyumba zinazouzwa, Mchechu alisema haulengi kuinufaisha NHC bali lengo lake ni kuwanufaisha wananchi wa hali ya chini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles