23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TPSF yataka mageuzi ya viwanda

Na Christina Gauluhanga, Dar es Salaam
SERIKALI imetakiwa kuharakisha mageuzi ya viwanda ili kukuza soko la biashara nchini na kuongeza pato la taifa.
Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti Mtendaji wa Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye, alisema maboresho ya viwanda yatasaidia bidhaa nyingi kununuliwa nchini.
Alisema kasi ya uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi imeongezeka ambapo mwaka huu zimefikia dola za Marekani bilioni 5 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo zilikuwa dola bilioni 4.
“Ukiagiza nje ya nchi ina maana unapunguza soko la ajira na pato la taifa, umefika wakati Serikali kuona umuhimu wa kuboresha viwanda vyetu ili bidhaa nyingi zizalishwe hapa hapa,” alisema Simbeye.
Aidha Simbeye alisema ziara zilizofanywa na Rais Jakaya Kikwete nje ya nchi zimeanza kuzaa matunda baada ya Tanzania kuanza kupokea wafanyabiashara wengi.
Alisema wafanyabiashara wa ngozi kutoka nje ya nchi wamewasili nchini kufanya mkutano na wafanyabiashara wa nchini ili kukuza uwezo.
Simbeye alisema Tanzania ni nchi ya tatu barani Afrika kwa uzalishaji wa ngozi.
Akizungumzia ubora wa bidhaa zinazozalishwa China, Simbeye alisema Watanzania wengi wanapenda bidhaa za bei nafuu, jambo ambalo limekuwa likichangia kuharibu soko la Tanzania.
“Ukienda nchi nyingine zipo bidhaa zinatoka China, lakini zina ubora wa hali ya juu kutokana na kuwa na viwango vizuri,” alisema Simbeye.
Naye Mwenyekiti wa China Africa Business Counsil tawi la Tanzania, Xian Ding alisema ushirikiano wa dhati kati ya nchi hizo umeanza kuzaa matunda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles