24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

ACT yatikisa ngome ya Sitta, Ukawa

Na Bakari Kimwanga, Tabora
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeviliza vyama vinavyoundwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya mamia ya wananchi wa Wilaya ya Urambo kutangaza kujiunga na chama hicho.
Wilaya ya Urambo ina jimbo moja la uchaguzi la Urambo Mashariki ambalo linaongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta (CCM).
Nia hiyo ya wana-Urambo ilimfanya Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kujikuta akibubujikwa na machozi ya furaha, huku kila mara akiwashukuru wananchi wa Tabora kwa kumfuta machozi kwa kukubali kuwa wazalendo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana mchana baada ya viongozi wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Anna Mghwira na Zitto kuzungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Wilaya ya Urambo.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Tarafani wilayani hapa na baadae Tabora mjini, Zitto alisema uamuzi wake wa kujiunga na chama hicho ulitokana na kuhusishwa na vitendo vya manyanyaso na kunyanyapaliwa na watu wasiomtakia mema katika chama chake cha awali.
“Ndugu zangu leo mmenifariji sina la kusema, nabaki nalia kwa machozi ya furaha, ninajua Urambo na Tabora ni mkoa wa kihistoria kuanzia kwa Mtemi Mirambo, Isike ambao walisimama imara kumwondoa mkoloni.
“Leo nimekuja kwenu kuwaletea jahazi hili la ACT-Wazalendo, ninawaomba mniunge mkono, tangu ulipoingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 Urambo ilichagua mbunge wa upinzani toka NCCR-Mageuzi na sasa sina hofu nanyi…umaskini sasa tuseme hapana,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles