33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Cheka atolewa jela, apewa kifungo cha nje

FRANCISI-CHEKANA RAMADHAN LIBENANGA, MOROGORO

BONDIA nguli nchini, Francis Cheka, jana alitolewa rumande na kupewa kifungo cha nje, huku akitakiwa kuripoti katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini kila siku kwa ajili ya shughuli za kijamii.

Februari 2, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mkoani hapa ilimhukumu Cheka kifungo cha miaka mitatu kwenda jela na faini ya Sh milioni moja, baada ya kumshambulia na kumdhuru meneja wa baa yake, Bahati Kabanda, kosa alilofanya Julai 2, mwaka jana.

Hatua hiyo ya Cheka kutolewa rumande imekuja baada ya kukata rufaa akiiomba mahakama impe kifungo cha nje kutokana na majukumu ya kifamilia aliyokuwa nayo, huku akidai anatategemewa kwa kila kitu na familia yake.

Hata hivyo, Cheka ametakiwa kutofanya kosa lolote ndani ya miaka mitatu ya kifungo chake, kwani akipatikana na hatia nyingine atarudishwa jela na kutumikia kifungo alichonacho mara mbili.

Mara baada ya kupata hukumu ya mwanzo, bondia huyo akizungumza na MTANZANIA alisema kifungo alichopewa kina mkono wa watu wenye lengo la kutaka kuchafua jina lake na maisha yake.

“Nimeshangazwa kusomewa kuwa nimekiri kosa la kumpiga mlalamikaji wakati katika maelezo yangu nilikana shtaka, hivyo ni wazi kesi hii ilipangwa kuvurugwa ili niweze kufungwa na kupotezwa katika ulimwengu wa wanamasumbwi,” alisema.

Hata hivyo, bondia huyo baada ya kutoka alikutana na familia yake, jamaa na marafiki ambao walijitokeza kumlaki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles