25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

HATA KAMA ANAKUPENDA, STORI HIZI ACHANA NAZO KABISA!

lovers

NIMEWAHI kuongelea jambo hili huko nyuma, lakini nalazimika kulirudia tena kwa ufafanuzi zaidi kwa ajili ya kuwasaidia vijana wenzangu wengi ambao wanajikuta wakiingia kwenye matatizo kwa kutojua aina sahihi za uhusiano.

Hivi karibuni kumeibuka mambo ya aibu kwa pea mbili za uhusiano, sababu ikitokana na kutokuwa makini katika uhusiano.

Yupo dada ambaye picha zake chafu zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kumdhalilisha. Huyu dada ameibuka na kufafanua kwa kina kilichotokea. Kwamba alikuwa katika uhusiano na kijana huyo na kwamba alipiga picha hizo kwa ridhaa yake, lakini baada ya kuachana, jamaa akaamua kuzisambaza na kumchafua (ingawa ukweli ni kwamba yeye na huyo jamaa wote wamechafuka).

Ukiacha huyo, kuna binti mwingine picha zake zikimwonyesha akiwa faragha na mwanaume zimetumwa kama zawadi siku yake ya harusi.

Baada ya kutoka katika fungate lao, wakati wanafungua zawadi, ndipo walipokutana na zawadi hiyo iliyogeuza ndoa yao kuwa machozi tupu.

Katika matukio hayo mawili, yanatoa picha ni kwa namna gani vijana tunapaswa kuwa makini sana katika uhusiano na wenzi wetu, kwani tunayoyafanya leo yanaweza kugeuka mwiba siku zijazo.

Je, upo kwenye uhusiano wa aina gani? Unafanya matendo gani katika uhusiano wako? Ipi mipaka ya kuzingatia kwenye uhusiano? Marafiki, ni kweli kwamba mapenzi ni upofu na wakati mwingine unaweza usikumbuke kuzingatia mambo muhimu, lakini ni vizuri kujipa nafasi ya kwanza.

Kuangalia zaidi kesho yako. Huyo uliyenaye huna uhakika wa kuwa naye maisha yako yote. Inawezekana unamwamini na unamjua vya kutosha, lakini nikuambie ndugu yangu, bado hujamfahamu kiasi cha kumpa thamani ya maisha yako yote.

Katika zama hizi za Sayansi na Teknolojia, uzungu umekuwa mwingi sana kwenye uhusiano. Kwa bahati mbaya, mazoea hayo yamekuwa tatizo katika jamii yetu.

Kutokana na wengi kujifanya wataalamu wa kuiga, wamejikuta wakitumbukia kwenye michezo michafu ambayo mwisho wa siku inaathiri afya zao.

Katika mada hii, nitachambua aina za mazoea mabaya na madhara yake, ambapo mwisho wa siku, kama ni mmoja wa walio katika michezo hiyo hatari, utaamua kusuka au kunyoa baada ya kumaliza kusoma mada hii.

 

KINYUME NA MAUMBILE

Mchezo huu umeingia kwa kasi sana kwenye jamii yetu. Waanzilishi wakuu wa ujinga huu ni wanaume. Kiukweli, baadhi ya wanawake wamejikuta kwenye wakati mgumu kwenye mapenzi, baada ya wanaume wengi kucharukia kuanza kufanya mapenzi kwa njia hii isiyokubalika.

“Kaka Shaluwa, mpenzi wangu ananing’ang’aniza sana nifanye naye huu mchezo, anasema eti amesikia marafiki zake wakisema tukifanya, eti mapenzi yataongezeka! Sijui kama kuna ukweli wowote, hebu niambie kaka yangu,” huyu ni msomaji wangu ambaye aliniomba ushauri kwa njia ya simu.

Ipo mifano mingi, lakini yupo dada mmoja aliwasiliana nami, akaniambia kwamba anafanya mchezo huo kwa mwaka wa tatu sasa kwa lengo la kulinda usichana wake. Nilizungumza naye mengi na kumweleza madhara makubwa ambayo anaweza kuyapata kwa kuendekeza mchezo huo.

Nashukuru alielewa na alisema ameachana kabisa na mchezo huo. Kifupi si tabia nzuri kuiendekeza na husababisha madhara makubwa sana kiafya.

 

ATHARI ZAKE NI ZIPI?

Zipo athari za moja kwa moja ambazo mhusika anaweza kuzipata kwa kuendekeza mchezo huu hatari. Kwanza inakupasa ujue kwamba, njia hiyo ni maalum kwa ajili ya kupitisha kinyesi tu na siyo kitu kingine chochote.

Mwanamke anaweza kupata magonjwa ya uambukizo ya njia ya haja kubwa. Mafuta mepesi yaliyopo kwenye njia hiyo muda wote kwa lengo la kupitisha kinyesi kirahisi, yatakauka kutokana na matumizi mapya ambayo mhusika atakuwa ameyaanza.

Kukauka kwa mafuta hayo husababisha choo kutoka kwa tabu na hatimaye kuacha mikwaruzo ambayo husababisha vidonda – mwisho wake kupata maambukizi ya virusi ambavyo humea siku zote kwenye njia hiyo.

Hii ndiyo sababu mwanamke hushauriwa kutawaza akianzia sehemu ya haja ndogo kuelekea haja kubwa ili kuepusha maambukizi ya virusi vilivyopo kwenye njia ya haja kubwa. Zaidi ya yote ni vidonda na maumivu makali wakati wa kupata haja kubwa.

Misuli inayodhibiti haja kubwa hulegea na hivyo kuwepo kwa hatari ya kutokwa na haja bila taarifa. Kwa maneno mengine, mfanyaji wa kitendo hicho anajiweka kwenye hatari ya kuanza kutumia nepi akiwa mtu mzima!

Zaidi ya yote, wakati wa kujifungua mwanamke hupata tabu kubwa kwa sababu hatakuwa na uwezo wa kusukuma mtoto na hivyo kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa kujifungua kwa njia ya upasuaji.

Wiki ijayo tutaendelea, tukianzia na madhara ambayo mwanaume anaweza kuyapata, USIKOSE!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles