24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

DAKIKA ZA MWISHO ZA RAIS YAHYA JAMMEH

Yahya-Jammeh

Na Mwandishi Wetu

WAKATI dunia ikiwa inasubiri kwa hamu juu ya uamuzi wa kuachia ngazi kabla ya kuvamiwa na majeshi ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) ya Ecomog, swali moja lilikuwa likiulizwa; ni wapi ambako atakwenda au ataamua kubaki ndani ya nchi yake rais aliyemaliza muda wake, Yahya Jammeh?

Kiongozi huyo kutoka Gambia amekuwa kwenye wingu jeusi la kisiasa nchini mwake tangu aliposhindwa uchaguzi mwishoni mwa mwaka jana, baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza kuwa mgombea wa Muungano wa vyama vya Upinzani, Adama Barrow kuwa mshindi wa kiti cha urais wa nchi hiyo.

Ushindi wa Barrow ulihitimisha utawala wa miaka 20 wa Rais Jammeh, ambaye amekuwa maarufu kote Afrika kutokana na vituko alivyonavyo.

Mara baada ya Tume kutangaza mshindi, Rais Jammeh alikubaliana na kushindwa kwake kwenye uchaguzi huo, kabla ya siku chache baadaye kubadili msimamo na kudai kulikuwa na kasoro mbalimbali kwenye zoezi zima la uhesabuji wa kura.

Tangu hapo, Jammeh alikataa kuondoka Ikulu ya nchi hiyo na kuing’ang’ania, hali iliyomlazimu Rais mteule Adama Barrow, kukimbilia nchini Senegal. Utawala wa Rais Jammeh ulifika kikomo Januari 19 wiki hii, lakini alikataa kuachia ngazi kinyume cha katiba ya Gambia iliyomtaka kukabidhi madaraka kwa rais mpya.

Kufuatia sintofahamu hiyo, Rais mteule wa nchi hiyo, Barrow, aliapishwa rasmi kuwa rais katika ofisi za ubalozi wa Gambia zilizoko jijini Dakar, nchini Senegal juzi Alhamisi na kutoa wito kwa wanajeshi kuonesha utiifu kwa Serikali yake.

Barrow, alilazimika kuapishwa nje ya nchi yake kutokana na kuhofia usalama wake pamoja na hatua ya Rais Jammeh kukataa kuondoka madarakani.

TISHIO LA KIJESHI

Kutokana na Rais Jammeh kukataa kuachia ngazi kwa hiari, viongozi wa nchi za Jumuiya ya Ecowas zilikubaliana kutomtambua kiongozi huyo na kumtaka aondoke kwa hiari. Aidha, Serikali ya Botswana ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), imekuwa nchi ya kwanza kutoka nje ya Afrika Magharibi kutangaza kutomtambua Jammeh.

Hatua ya kubaki madarakani imesababisha Nigeria na Senegal kuandaa majeshi ya kumtoa Jammeh kwa nguvu, huku mkuu wa majeshi wa nchi hiyo akikataa kuliamrisha jeshi kupambana na wananchi ambao wamekuwa wakiandamana kila siku.

Majeshi ya Senegal yamepiga hatua zaidi kwa kuvuka mpaka na kuingia nchini Gambia Januari 19 mwaka huu na baadaye walisimamisha operesheni yao kwa jaribio la mwisho la kumshawishi Yahya Jammeh.

Jana Rais wa Guinea, Alpha Conde, alitarajiwa kufanya ziara nchini Gambia kwa minajili ya kumshawishi Jammeh kuachia ngazi.

Jaribio la mwisho katika kumwelewesha Jammeh kuachia ngazi kwa amani lilifanyika jana Ijumaa, Mwenyekiti wa Tume ya Ecowas, Alain Marcel de Souza, alitangaza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dakar, nchini Senegal.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles