26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MKE AMVUNJA MGUU MUMEWE

early_african_maasai_tribal_rungu_war_club_early_to_mid_20th_c__1_lgw

Na Walter Mguluchuma-Katavi

MKAZI wa Kijiji cha Uzega Tarafa ya Inyonga  wilayani  Mlele mkoani Katavi, Mashaka   Kianga,  amejeruhiwa vibaya mguu wake wa kushoto hadi kuvunjika, baada ya kupigwa na  rungu na mke wake mkubwa wakati  alipokuwa  akiamua ugomvi wa wake  zake, mkubwa na  mdogo waliokuwa wakigombea mifuko mitupu ya mbolea ya tumbaku.

Tukio hilo la mume kupigwa rungu na mke  wake mkubwa, lilitokea juzi saa nne asubuhi   katika Kijiji cha Uzega.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Abel Kalifumu, alisema kabla ya Mashaka  kujeruhiwa, aliwakuta wake zake wakiwa  wanapigana kugombania mifuko mitupu ya  mbolea ya tumbaku aina ya NPK.

Alisema ugomvi wa wanawake hao ulianza     baada ya mke mkubwa kumtaka mke mdogo  ampatie mifuko hiyo, hata  hivyo  mke  mdogo  alimkatalia ndipo ugomvi ulipoanza.

Kalifumu alisema wakati wanaendelea na   ugomvi, mume wao aliwakuta wanaendelea kupigana, jambo lililoonekana kumkasirisha.

Mashaka alichukua fimbo na kuanza  kuwacharaza viboko kwa  lengo la  kuwaamua, ndipo mke mdogo alivyoona viboko   vimemzidia aliamua kukimbia na kumwacha  mwezake eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles