26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

NGOZI RASILIMALI INAYOPUUZWA

Ngozi ya ng'ombe iliyochakatwa
Ngozi ya ng’ombe iliyochakatwa

Na Joseph Lino,

Tanzania ina utajiri wa mifugo ambayo haijaweza kustawi vizuri katika kuinua hali ya maisha ya wananchi wengi wanaofuga kutokana na uhafidhina.

Kwa sababu hiyo, malighafi nyingi zinazotokana na mifugo hupotea na kutopewa kipaumbele, hali inayosababisha wafugaji kutofaidika na sekta hiyo.

Tanzania ni nchi ya pili Afrika kuwa na mifugo wengi ambao ni moja ya sekta yenye tija ya kuleta maendeleo nchini.

Ngozi ni moja ya mazao yanayotokana na mifugo, lakini sekta ya ngozi bado ipo nyuma kimaendeleo kama walivyo wenye mifugo hiyo.

Kwa mujibu wa Jukwaa Huru la Wadau wa Kilimo (ANSAF), kuna viwanda tisa vya kusindika ngozi zenye uwezo wa kuchakata ngozi mita za mraba milioni 40 kwa mwaka, hata hivyo viwanda hivyo vina uwezo mdogo wa kusindika malighafi inayopatikana nchini.

ANSAF inasema  ngozi za ng’ombe 4,643,000 pamoja na ngozi  za mbuzi na kondoo  22,820,000 husindikwa kila mwaka, lakini husindikwa  kwa kiwango cha chini.

Sekta ya ngozi bado haijaendelezwa kwa kiasi kikubwa ambacho kwa sasa sekta hiyo imetengeneza ajira chache ikilinganisha na mifugo iliyopo nchini.

Kwa  mfano, wastani uzalishaji wa ng’ombe 1,000 na mbuzi 1,500 ambao huchinjwa kila siku katika machinjio ya Dodoma Mjini.

ANSAF inaelezea kuwa kiasi cha Sh milioni 15 kuhitajika kujenga kiwanda cha kusindika bidhaa za ngozi.

“Ngozi ya ng’ombe hununuliwa kwa Sh 8,000 na ya mbuzi Sh 2,000 na ikisindikwa huuzwa Sh 40,000 na matokeo yake kutengeneza viatu jozi nne,” inaeleza ANSAF.

Kwa mantiki hiyo, mtu anaweza kutengeneza jozi  30 au 35 ambazo zinaweza kuuzwa Sh milioni 1.75 kila mwezi.

Nafasi ya Tanzania  kuwa na idadi nyingi ya mifugo Kusini mwa Jangwa la Sahara, hivyo ina uwezo wa kuuza viatu na bidhaa zote zinazotokana na ngozi masoko ya nje.

ANSAF inapendekeza kwamba Serikali iingie mikataba na makampuni ya nje ambayo yanaweza kutengeneza ajira na kuchangia kwenye Pato la Taifa.

Kwa takwimu ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inaonesha katika mwaka 2015/16, vipande ghafi 187,000 vya ngozi za ng’ombe vyenye thamani ya Sh bilioni 2.4 na vipande ghafi 124,000 vya ngozi za mbuzi/kondoo vyenye thamani ya Sh milioni 121.5 viliuzwa nje ya nchi.

Aidha, ngozi zilizochakatwa ni vipande 1,575,139 vya ng’ombe vyenye thamani ya Sh bilioni 45 na vipande vya ngozi za mbuzi/kondoo 1,124,000 vyenye thamani ya Sh bilioni 7.5.

Kwa upande mwingine, mifugo iliyouzwa ndani kupitia minadani ni ng’ombe 1,470,805, mbuzi 1,161,840 na kondoo 253,243 wenye thamani ya Sh bilioni 976.474.

Katika mwaka 2015/16, idadi ya mifugo nchini inafikia ng’ombe milioni 25.8, mbuzi milioni 17.1 na kondoo milioni 9.2.

Hata hivyo, uzalishaji wa nyama umeongezeka kutoka tani 597,757 (ng’ombe 319,112; mbuzi na kondoo 124,745, nguruwe 54,360 na kuku 99,540) mwaka 2014/2015 hadi tani 648,810 (ng’ombe 323,775; mbuzi na kondoo tani 129,292).

Takwimu hizo zinaonesha kuwa juhudi  zinafanywa na wadau pamoja na Serikali kuongeza mazao yatokanayo na mifugo, haswa   ng’ombe lakini  inaonesha bado iko chini sana  kwani wafugaji wengi hawajaenda shule na wana utamaduni wa  kujali sana uwingi kuliko ubora wa mifugo hiyo.

Watu wa makamo wanakumbuka wakati  wa awamu ya kwanza ya utawala wa nchi chini  ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati  ng’ombe kulikuwa na kampuni mahiri saba zinamshughulikia.

Kurudia mwenendo huo si kosa ila tutafanikiwa vilivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles