31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

HALI IKIENDELEA HIVI YANGA WASAHAU UBINGWA MSIMU HUU

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


yanga_sc_lineupTIMU ya Yanga inaweza kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu iwapo uongozi wa klabu hiyo utafanya uamuzi mgumu na wa haraka katika benchi lao la ufundi kabla hali haijawa mbaya.

Ni muda sasa tangu uongozi wa klabu hiyo ufanye mabadiliko ya benchi hilo, lakini kumekuwa na hali isiyoridhisha hasa baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo mbaya wa matokeo tangu waajiri kocha mpya.

Kwani ni vigumu kuliona hili lakini hali si shwari kati ya kocha mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina na Mkurugenzi wa benchi la ufundi la timu hiyo, Hans van Pluijm.

Kwa mbali unaweza kuona kama kuna amani, lakini ukweli ni kwamba Pluijm hana furaha kabisa kutokana na nafasi yake kupewa mtu mwingine.

Na hali ikiendelea kuwa hivi inaweza kutoa nafasi kwa mahasimu wao, Simba ambao kwa sasa ndio vinara wa ligi hiyo.

Yanga kwa sasa ni kama bomu linalofukuta chini chini lakini ipo siku litakuja kulipuka kutokana na kinachoendelea katika klabu hiyo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo, zinaeleza kuwa Pluijm ndiye chanzo cha vita inayoendelea kwa sasa.

Hali hiyo imesababisha kutokuwepo na utulivu kwa baadhi ya viongozi wa Yanga ambao wanadai Pluijm anasababisha makundi kwa wachezaji na kupelekea baadhi yao kutojituma kwenye timu.

Mmoja wa viongozi wa kamati ya usajili ya klabu hiyo anasema: “Hans haelewani na Lwandamina, kuna ‘bifu’ zito kati ya wawili hao.

“Bifu hilo limepelekea uongozi wa Yanga kukaa kikao cha kutaka kumwondoa Pluijm lakini kuna baadhi ya viongozi bado wanamtaka Pluijm, lakini wapo ambao wanasema kwamba iwapo  ataendelea watajiuzulu nafasi zao.”

Miongoni mwa wanaomtetea Pluijm ni bilionea wa klabu hiyo ambaye anaonekana kumng’ang’ania Mholanzi huyo.

Zaidi ni kwamba, bifu la viongozi hao wa benchi la ufundi la Yanga linaweza kuiathiri timu hiyo hata katika Ligi ya Mabingwa Afrika Februari mwaka huu.

Binafsi ningependa kuona viongozi wa klabu hiyo wakichukua uamuzi wa haraka ili kuisaidia timu hiyo kabla ya kuanza kwa michezo ya kimataifa.

Bado kuna nafasi ya kutosha kwa viongozi hao kuliangalia kwa umakini suala hili, licha ya mara kadhaa kusisitiza kwamba hakuna bifu ndani ya klabu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles