31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MSN WAFIKISHA MABAO 300 BARCELONA

BARCELONA, HISPANIA


 

MSNWASHAMBULIAJI hatari wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, wamefanikiwa kufikisha mabao 300 tangu watatu hao walipoanza kucheza pamoja ndani ya klabu hiyo.

Juzi klabu hiyo ilishuka dimbani katika mchezo wa Copa del Rey dhidi ya wapinzani wao Athletic Bilbao, ambapo Barcelona imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali baada ya kushinda mabao 3-1 na kuifanya iwe na jumla ya mabao 4-3, baada ya mchezo wao wa awali Athletic Bilbao ikishinda mabao 2-1.

Mabao hayo ya Barcelona yalifungwa na nyota hao watatu, huku bao la Athletic Bilbao likifungwa na nyota wao, Enric Saborit, lakini kwa upande wa nyota hao wa Barcelona wameweka historia ya kuwa na jumla ya mabao 300 baada ya kila mmoja kufunga katika mchezo huo wa juzi.

Wakati huo nyota wa Barcelona, Messi, amefikisha jumla ya mabao 31 ya kupigwa kwa mpira wa adhabu tangu kuanza kwa soka lake la kimataifa, wakati huo bao lake la juzi la mpira wa adhabu likiwa la 26 na kufikia rekodi ya kocha wa sasa wa klabu ya Everton, Ronald Koeman, ambaye alifunga wakati akiwa mchezaji.

Kocha huyo wa Everton wakati anacheza soka alikuwa anacheza nafasi ya kiungo na wakati mwingine alikuwa anacheza nafasi ya ulinzi, lakini tangu anaanza soka hadi anastaafu alicheza jumla ya michezo 613 ya klabu na timu ya taifa huku akifunga jumla ya mabao 207.

Koeman kupitia akaunti yake ya Instagram, haraka alimpongeza Messi kwa kufikia rekodi yake ya mabao 26 ya mipira ya adhabu. “Hongera sana Messi kwa kufikisha mabao 26 ya mipira ya adhabu, ninaamini rekodi hiyo utaivunja,” aliandika Koeman.

Kwa upande mwingine bao ambalo lilifungwa na Suarez, lilimfanya afikishe bao lake la 100 tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2014 akitokea timu ya Liverpool ya nchini England.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles