27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WALIOMCHARAZA VIBOKO MWANAMKE WAKAMATWA

o-black-man-handcuffs-facebook

Na ASHA BANI, DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi limewakamata watuhumiwa 10 kwa  kuhusika na tukio la kumchapa viboko na kumdhalilisha hadharani mwanamke mwenye umri wa miaka 38 (jina tunalo) mkoani Mara.

Kati ya watuhumiwa hao, watano ni viongozi wa Baraza la Kimila la Kabila la Wasimbiti, akiwamo mwenyekiti na wajumbe wanne.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Mkoa wa Polisi Tarime/Rorya, Andrea Satta, tukio hilo lilitokea Desemba 23, mwaka jana saa 11 jioni eneo la Mastooni katika Kitongoji cha Migitu, Kijiji cha Kinesi, Kata ya Nyamunga ambako mwanamke huyo alishambuliwa kwa viboko na watu sita walioamrishwa kumchapa hadharani.

Pia wajumbe 10 wa Baraza la Mila la Kabila la Wasimbiti liitwalo Irienyi, liliamuru adhabu hiyo baada ya kulalamikiwa na kupelekwa barazani hapo na mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 55, kuwa mwanamke huyo alimtukana na aliahidi kumuua kwa kutumia uchawi.

Baada ya malalamiko hayo, baraza hilo liliamuru vijana hao kumchapa viboko mwanamke huyo wakimtuhumu kumtusi mama yake mzazi.

Kamanda huyo alisema baadhi ya matusi yaliyoandikwa katika taarifa ya baraza hilo la kimila ni pamoja na mwanamke huyo kumkana mama yake kuwa si mama yake mzazi.

Taarifa ya polisi ilieleza kuwa watuhumiwa wengine wanne walishiriki  kumshika na kumlaza mwanamke huyo ili apate  adhabu hiyo ya viboko.

“Mtuhumiwa mmoja ndiye aliyeshiriki moja kwa moja kumchapa muathirika huyo, hivyo watuhumiwa wote kwa pamoja wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano na jitihada zaidi za kuwadaka watuhumiwa hao zinaendelea,’’ ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa za tukio hilo zilianza kusambaa kupitia mitandao ya kijamii, huku watu mbalimbali wakipinga unyanyasaji huo.

Kupitia ukurasa wake wa Istagram, msanii wa bongo fleva maarufu kwa jina la Ney wa Mitego, alionyesha kusikitishwa na tukio hilo, huku akisema licha ya ubabe na ukorofi wake katika maisha yake, hakuwahi kumpiga mwanamke.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles