27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

SHULE 15 ZAPEWA VIFAA VYA SH MILIONI 50

ndalichako

Na CLARA MATIMO, MWANZA


 

SHULE za msingi  15 za  Serikali  zilizopo Halmashauri ya Jiji la Mwanza, zimepatiwa msaada  wa vifaa mbalimbali vya sekta ya  elimu vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 50  kutoka  shirika  la Brac Maendeleao Tanzania, tawi la Mwanza.

Shirika hilo, limetoa msaada huo ikiwa ni utekelezaji wa mradi  wa kuwasaidia watoto wa kike   wanaokumbwa na changamoto, wakati wa masomo ‘Girls Education Challenge (GEC) ulioanza  kutekelezwa tangu  mwaka 2014 katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Singida, Tabora na Dar es Salaam.

Shule zilizopatiwa msaada huo, ni Iseni, Amani, Nyabulogoya, Pamba B na C, Mabatini A na C, Bugarika, Miembeni, Nyakabungo, Lake, Nyashana, Nyakurunduma, Tambuka Reli na Mbungani.

Akizungumza   wakati  wa hafla ya kukabidhi  vifaa hivyo  mwishoni mwa wiki  iliyopita kwa Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, Meneja   Mradi  wa GEC,  Kanda ya Ziwa,  Shahinoor Rahman, alisema  lengo la mradi huo ni kuwasaidia watoto wa kike waliokata tamaa ya kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles