24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WATU 200 WAKAMATWA KWA UJANGILI

tembo

Na ASHA BANI-MOROGORO

WATU zaidi ya 200 wamekamatwa katika kipindi cha mwaka jana kutokana na makosa ya kukutwa na nyara mbalimbali za Serikali.

Pia zaidi ya Sh milioni 800 hadi 900 zilipatikana kutokana na faini za watu wanaokutwa na nyara za Serikali sambamba na walioshindwa kulipa faini kufungwa miaka 20-25.

Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Makosa ya Jinai (DPP), Biswalo Mganga wakati akizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA) walipokutana  wahifadhi wakuu kwa lengo la kuweka mkakati wa udhibiti wa ujangili.

Alisema kati ya watuhumiwa hao endapo wote wangefanikiwa kutoa faini na kutofungwa, kiasi cha Sh bilioni 164 zingekusanywa na kwamba hiyo inaonyesha ni jinsi gani udhibiti unaendelea kwa kasi.

Biswalo alisema kutokana na takwimu hizo, kwa mwaka huu hawatategemea kutokea tena kwani idadi hiyo ilikuwa kubwa na inatisha kwa Taifa.

Alisema kila mmoja ana jukumu la kulinda maliasili za Serikali, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za wahalifu hao ili ziweze kushughulikiwa haraka na kufunguliwa mashtaka.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, alisema Serikali imeweka mpango mkakati mpya kuhakikisha ujangili unaendelea kudhibitiwa kwa hali ya juu.

Kutokana na hali hiyo, amewataka watumishi wa TAWA kutojifungia maofisini na badala yake kuingia kufanya kazi katika maeneo yao ya kazi na hapo ndipo mafanikio yatatokea.

“Kuna haja ya kujitathimini upya, sio muwe viongozi wa ofisini tu. Mnatakiwa muwe ‘field’ pamoja na mabosi zenu, na kama kuna kitu kinahitajika maamuzi yake yatolewe kwa muda mwafaka,’’ alisema Meja Milanzi.

Alisema kila mfanyakazi na kila mtu aliyepo katika mamlaka hiyo, anatakiwa kujitafakari kwa utendaji wake.

“Ujangili umepungua kwa kiasi kikubwa na pembe au meno ya ndovu yanayokamatwa sasa ni masalia ya zamani na ndiyo maana hata wanyama wanaoonekana kufa hawapo kwa sasa, hii ni jitihada na juhudi kubwa ya ulinzi ,’’ alisema Milanzi.

Katika hatua nyingine, amepongeza hatua ya nchi ya China kuua soko la manunuzi ya meno ya tembo, jambo ambalo alisema litafanikisha zaidi ujangili kupungua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles