24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

WANANE WAKAMATWA KWA UJANGILI SERENGETI

c56b0985-6349-48fe-99a8-f7bfd5314b25_mw1024_s_n

Na MALIMA LUBASHA- SERENGETI

Wakazi wanane wa vijiji vya Kibeyo wilayani Serengeti mkoani Mara, wamekamatwa na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya kwa tuhuma za kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kufanya vitendo vya ujangili.

Mwendesha Mashtaka wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Emmanuel Zumba, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ismael Ngaile, aliwataja washtakiwa hao  ni Amos Chacha (22), Marwa Ghati (20) na Nyabare Chacha (18)   waliokamatwa Desemba 19, mwaka jana, huku wakiwa na  vipande vitatu vya nyama kavu ya Swala Impala vyenye thamani ya Sh 858,000.

Wengine ni Mniko Gesaro (30), Silasi Silasi (30), Chacha Kibone (30) na James Thomas (20) ambao walikamatwa  siku hiyo hiyo eneo la Borogonja ndani ya hifadhi hiyo.

Baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka matatu yanayowakabili  walikana kuingia ndani ya hifadhi kinyume cha sheria hivyo hakimu aliamuru warudishwe mahabusu hadi kesi itakapotajwa Januari 3,2017.

Katika hatu nyingine, mahakama hiyo ilimuhukumu Chacha Itembe(40) mkazi wa Kijiji cha Kibeyo Kata ya Kisangura Tarafa ya Rogoro kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela na kulipa faini ya Sh 200,000 baada kutiwa hatiani kwa kosa la kuingia ndani ya hifadhi bila kibali na kupatikana na silaha.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ismael Ngaile, alisema ametoa adhabu hiyo baada ya mshtakiwa kukiri kosa mwenyewe hivyo kuirahisishia mahakama kutoa adhabu na kulipa faini ya Sh 100,000 kwa kila kosa.

Hakimu Ngaile, alisema kosa la kwanza la kuingia ndani ya hifadhi bila kibali kinyume na kifungu cha 21(1) na (2) sura ya 29 kifungu (1) namba 11 ya mwaka 2003 kifungo ni mwaka mmoja na faini ya Sh100,000 na kosa la pili la kupatikana na silaha kisu , nyaya 3 za kunasia wanyama hifadhini kinyume na kifungu namba 24(1) (b) na (2).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles