23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAFANYABIASHARA SOKO LA BONANZA HAWANA CHOO

p1240119

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA 

WAFANYABIASHARA katika soko la Bonanza la mkoani hapa wanalazimika kujisaidia katika nyumba jirani na soko hilo kutokana na soko hilo kukosa vyoo.

Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa jana, Mwenyekiti wa soko hilo, Goha Magwayi alisema soko hilo lina jumla ya wafanyabiashara 500 ambao wamekuwa wakiteseka kutokana na kukosa huduma hiyo.

Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ilitenga zaidi ya Sh milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa choo miaka sita iliyopita lakini hadi sasa choo hicho ujenzi umesimama.

“Hapa tuko wafanyabiashara wa samaki, matunda na mbogamboga, Serikali inatuangalia tu kikitokea kipindupindu wanakuja na kuuliza sababu ni nini wakati ukweli upo wazi hakuna vyoo.

“Manispaa ndiyo hatuielewi kabisa tunahisi kuna wajanja wamepiga fedha kupitia ujenzi wa hiki choo, kwa nini tuumie sisi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles