27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI ITAMLINDA MTOTO WA KIKE – MAJALIWA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa.

Na Mwandishi Maalumu-LINDI

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa kike na ndiyo maana inasisitiza waachwe wasome hadi wamalize kidato cha sita.

Kauli hiyo aliitoa jana kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo.

Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

“Tumesema mtoto wa kike aachwe asome hadi kidato cha sita, akifika chuo kikuu atakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yake. Lakini kwa sasa waacheni watoto wa kike wasome. Ninyi vijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela,” alisema.

Alisema nia ya Serikali ni kupata watumishi ambao ni wataalamu wa kada tofauti kama madaktari, wanasheria, mafundi, walimu na hata wakuu wa wilaya ambao ni wanawake.

Aliwaonya wazazi wanaokubali kuongea pembeni (kupewa fedha) na wanaume waliowapa mimba mabinti zao, na kuwaeleza kuwa kwa mujibu wa sheria ilivyo, nao pia wanastahili kupewa adhabu ya kifungo jela.

“Mzazi ukigundua binti yako ana ujauzito toa taarifa haraka ili mhusika akamatwe mara moja. Usikubali kuongelea jambo hili pembeni, nawe pia utawekwa ndani pamoja na huyo mhusika ambaye tayari ni mhalifu.

“Mwanao akisema anataka kuoa, mzazi inabidi upeleleze kwanza anataka kumuoa nani. Asije kuwa anamuoa binti ambaye bado anasoma na akisema anaoa na wewe ukamkubalia tu, ikija kubainika kuwa ni mwanafunzi, wewe na mkeo mnakwenda jela,” alisema Majaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles