27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kigogo mbaroni kwa mauaji ya albino

NA PETER FABIAN, MWANZA
KIONGOZI wa chama kimoja cha siasa mkoani Mwanza (jina tunalo) anashikiliwa na Jeshi la Polisi akihusishwa na uhalifu wa utengenezaji wa noti bandia, utekaji na mauaji ya albino katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa.
Habari za uhakika zilizolifikia MTANZANIA kutoka vyanzo vyetu vya habari zimesema kuwa kigogo huyo alikamatwa wilayani Magu Februari 26, mwaka huu saa 7:00 usiku.
Kigogo huyo ambaye anadaiwa kuhusishwa na utekaji wa mauaji ya albino alikamatwa baada ya kutajwa na washirika wake katika matukio waliyofanya katika sehemu mbalimbali za mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Habari zaidi zilieleza kuwa kigogo huyo anahusishwa kwa karibu na matukio ya hivi karibuni yaliyotokea katika mikoa ya Mwanza na Geita ambako watoto wawili Pendo Emmanuel (4) mkazi wa Ndami Kwimba (Mwanza)na Yohana Bahati (1) wa Ilyamchele, Chato mkoani Geita.
“Mtuhumiwa alikamatwa na makachero wa polisi nyumbani kwake kabla ya kusafirishwa hadi Mwanza anakoshikiliwa hadi sasa na wakati anapekuliwa nyumbani kwake alikutwa na noti bandia,” kilieleza chanzo chetu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola alipoulizwa alisema kwa sasa yuko nje ya ofisi, hawezi kuthibitisha na kuahidi hadi atakapokuwa ofisini leo.
“Taarifa hiyo unayoniuliza kwa sasa sina, sina taarifa hiyo na siwezi kuizungumzia, kwa sasa niko nje ya ofisi naomba tuwasiliane (kesho) leo,”alisema Mlowola.
Februari 14 mwaka huu wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema watuhumiwa 15 wanaodaiwa kuhusika kumteka na kumsafirisha Pendo Emmanuel hadi hoteli moja jijini hapa walikuwa wakishikiliwa na Polisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles