33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WANAKIJIJI 300 WACHARAZWA VIBOKO NA SUNGUSUNGU

fimbo

Na KADAMA MALUNDE-SHINYANGA

ZAIDI ya wananchi 300 wakazi wa Kijiji cha Welezo Kata ya Nsalala wilayani Shinyanga mkoani hapa, wameshambuliwa kwa kuchapwa viboko sehemu mbalimbali za mwili na wengine silaha za jadi na walinzi wa Jeshi la Jadi (sungusungu) wapatao 800.

Tukio hilo linadaiwa kufanyika Desemba 10, mwaka huu kati ya saa 3:40 hadi 4:00 asubuhi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Welezo wakati sherehe za kusimika upya jeshi hilo la jadi la Kijiji cha Walezo (Kusebya) kufuatia kutengwa na kutozwa faini ya Sh milioni 1.3 kwa kosa la kukiuka maagizo ya sungusugu.

Wakizungumza juzi katika mkutano wa hadhara kuelezea ukatili waliotendewa na walinzi hao wa jadi, mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro, baadhi ya wanakijiji hao walisema siku hiyo walipaswa kujadiliana namna ya kuondolewa adhabu ya faini ya Sh milioni 1.3 katika mkutano ulioitishwa na viongozi wa sungusungu ngazi ya tarafa na wilaya.

Walisema katika mkutano huo badala ya kujadiliana namna ya kuwaondolea adhabu hiyo, walishangazwa kuamuliwa na viongozi wao wanaume kuvua mashati na wanawake kutoa vilemba kichwani na kukaa chini na kuinamisha vichwa ardhini na kuweka mikono yao nyuma ya kichwa.

Nkanda Hussein alimweleza mkuu wa wilaya mbele ya wanakijiji wenzake kuwa,  kumbe uongozi wa kijiji chao pamoja na ule wa sungusungu ulikuwa umealika askari wa jadi 800 kutoka vijiji jirani wakielezwa kuwa ulikuwa mkutano wa kushughulikia wahalifu sugu.

“Baada ya kuambiwa kukaa chini na kuinamisha vichwa chini, Mwenyekiti wa Sungusungu Wilaya ya Shinyanga, Kulwa Masanja, alianza kutaja majina ya wanakijiji wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kukata mapanga wazee vikongwe na wizi,” alisema.

“Kamanda alianza kuita majina ya watu waliodaiwa kuwa ni wahalifu na kuwataka wajitokeze mbele ya mkutano, ambapo walitakiwa kuchapwa viboko au kulipa faini ya Sh 200,000 kila mmoja,” alieleza Hussein.

Alisema baada ya watuhumiwa wanne kati ya 36 waliotajwa kuhusika na uhalifu na kugoma kupigwa, ndipo vurugu zilipoanza na Kamanda wa Sungusungu wa wilaya kutoa amri ya wanakijiji wote kucharazwa viboko na wengi walichapwa, huku baadhi wakipoteza fahamu na kukimbizwa kituo cha afya cha Tinde kupatiwa matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles