31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DK. NCHIMBI ALIPONGEZA SHIRIKA LA NYUMBA NHC

 MKUU  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi.
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi.

Na Mwandshi Wetu, Singida 

MKUU  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, amelishukuru Shirika la Nyumba  Taifa (NHC) kwa msaada wa mifuko ya saruji 10, kofia za bati 20, mabati 90 ya geji 28 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 2.6 milioni ukiwa ni msaada kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa bweni la Sekondari Mwanzi iliyoko wilayani Manyoni, mkoani Singida.

Dk. Nchimbi ametoa shukrani hizo juzi wakati akipokea msaada huo kutoka kwa Meneja wa NHC Mkoa wa Singida, Ladislaus Bamanyisa, na kutoa wito kwa mashirika, watu binafsi na taasisi zikiwamo mabenki, kuiga mfano mzuri wa NHC kusaidia Serikali katika kuboresha sekta mbalimbali ikiwamo ya elimu.

“Mimi nitumie nafasi hii kuwaita au kuwaalika mabenki na taasisi nyingine kuja mkoani Singida kutuunga mkono katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi, pamoja na uboreshaji wa miundo mbinu ya shule za msingi na sekondari,” alisema.

Ameongeza kuwa benki, shirika au watu binafsi watakaojitokeza kuunga mkono kuuendeleza Mkoa wa Singida kwa kujenga jengo lolote pamoja na majengo ya shule, huduma za afya na mengine yanayolenga kuwanufaisha wananchi, wataruhusiwa kupaka rangi na kuweka nembo zao ili kutangaza shughuli au huduma wanazotoa.

Amesema kwa njia hiyo benki, taasisi au watu binafsi watakuwa wamejitangaza na tangazo hilo litadumu kwa muda mrefu ikilinganishwa na matangazo mengine.

“Kwa upande wa wadau binafsi na wao wataruhusiwa kuweka picha za familia zao kwenye majengo au miradi husika. Kama ni mfugaji na ameuza sehemu ya mifugo yake kugharamia miradi wa umma, ataruhusiwa kuweka picha ya familia na ng’ombe zao,” amesema Dk. Nchimbi.

Naye Meneja wa NHC Mkoa wa Singida, Ladislaus Bamanyisa, amesema wataendelea kuiunga mkono Serikali katika kuboresha sekta mbalimbali na huo mchango ni sehemu ndogo ambapo shirika bado linaendelea na jitihada za kukusanya michango mingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles