28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

NJIA ZA KUKUMBUKA KITU UNACHOJIFUNZA

Uwezo wa kutunza kumbukumbu huweza kuonekana pia katika masomo.
Uwezo wa kutunza kumbukumbu huweza kuonekana pia katika masomo.

Na JOACHIM MABULA,

KUMBUKUMBU hufanya maisha yetu yawe ya kufurahisha. Kama tusingeweza kukumbuka mambo mbalimbali basi kila siku inapoanza tungekuwa na mwanzo mpya. Isingewezekana hata kujijua pale unapojitazama kwenye kioo.

Mambo na matukio ya kila siku hayangehusiana na wakati uliopita na wakati ujao, hatungejifunza kutokana na mambo yaliyopita au kutarajia wakati ujao. Watu wote wana uwezo wa kukumbuka bila kujali viwango vyao vya elimu.

Hatua tatu zinahusika katika kukumbuka: kuchanganua, kuhifadhi na kutumia. Ubongo wako huchanganua habari unapoitambua. Kisha habari hiyo inaweza kuhifadhiwa ili itumiwe wakati ujao. Mtu anaposahau moja kati ya hatua hizo tatu huwa imekatizwa.

Kuna aina mbalimbali za kumbukumbu, ambazo ni kumbukumbu hisi, kumbukumbu ya muda mfupi na kumbukumbu ya muda mrefu. Kumbukumbu hisi hupata habari kupitia kuchochewa kwa vipokezi vya hisi kama vile kunusa, kuona na kugusa. Kumbukumbu ya muda mfupi huhifadhi habari chache kwa muda mfupi.

Ikiwa ungependa kuhifadhi habari kwa muda mrefu zaidi, habari hiyo lazima ihifadhiwe kwenye kumbukumbu yako ya muda mrefu. Kama unataka kujifunza kitu chochote, unahitaji aina mbili za maarifa ya awali: maarifa kuhusu somo husika, kama hesabu, historia, au programu zake na maarifa kuhusu jinsi ya kujifunza.

Hata hivyo mfumo wetu wa elimu una kawaida ya kupuuzia kimojawapo, kitu ambacho ni hatari, kutokana na kwamba uwezo wako wa kujifunza ni kama kiashiria kikubwa cha mafanikio katika maisha, kuanzia kufanikiwa katika masomo hadi katika kazi. Yote yanahitaji kubobea kwenye ujuzi mmoja baada ya mwingine.

“Wazazi na waelimishaji wako vizuri katika kupasha aina ya kwanza ya elimu,” mwandishi wa Saikolojia Annie Murphy Paul. “Tupo vizuri kuzungumza kuhusu taarifa kamili; majina, tarehe, namba, kweli mbalimbali. Lakini mwongozo tunatoa kwenye kitendo cha kujifunza chenyewe hautegemeki kwa kuwa ni wa kubahatisha”.

Utafiti mpya wa elimu unaonyesha kwamba wanafunzi wanaopata alama za chini wana mapungufu makubwa katika uelewa wao wa mikakati ya utambuzi inayoruhusu watu kujifunza vizuri. Paulo anasema, hii inaweza kuwa sehemu ya sababu ya wanafunzi kufanya vibaya ni kwa kuwa hawajui mengi kuhusu jinsi ya kujifunza.

Henry Roediger na Mark McDaniel, wanasaikolojia katika Chuo Kikuu cha Washington mjini St. Louis na waandishi wa Make It Stick, wanasema “Jinsi sisi hufundisha na kutafiti kwa kiasi kikubwa ni mchanganyiko wa nadharia, tamaduni za kujifunza na uwezo wa utambuzi.”

Zifuatazo ni njia za kukumbuka mambo mbalimbali unayojifunza.

Jilazimishe kukumbuka

Kitu kidogo kinachoshangaza katika kujifunza kwa ufanisi ni kwamba ni vigumu kujifunza. Waandishi wa “Make It Stick” wanasema kuwa kama kujifunza ni kugumu kunafanya kujifunza kwako kuwa bora, kwa kuongeza uzito katika ukomo wa uwezo wako wa kujifunza na kukufanya imara.

Ni rahisi, ingawa si rahisi, kwa kuchukua fursa hii ya kujilazimisha kukumbuka. Kadi ya maelezo (flashcards) ni mshirika mkubwa katika hili, kwa vile kadi hizi hukulazimisha kutoa majibu baada ya kuona alama au picha fulani.

Usichukulie mambo kwa wepesi

Wakati unasoma kitu na unahisi ni rahisi sana, hapo kinachokutokea ni ufasaha. Urahisi huo utakuweka kwenye matatizo kwa maana kutakufanya kutochukulia mambo kwa uzito.

Kwa Mfano: Upo katika uwanja wa ndege wa Amsterdam na unajaribu kukumbuka namba ya lango la ndege yako ya Tanzania ili uende kusubiri hapo. Ukiangalia kwenye runinga za uongozaji unaona ni B44. Unapoina unafikiri B44, hiyo ni rahisi mno. Kisha unaendelea kutembea, mara unaangalia simu yako na papo hapo unajikuta umesahau wapi utaenda.

Unapaswa kusoma namba ya lango. Kisha ondoa macho kwenye runinga ya uongozaji na jiulize, ni namba gani ya lango? Kama unaweza kukumbuka kuwa ni B44, basi waweza kuendelea na safari yako.

Unganisha jambo jipya na mambo ya kale

Kwanza inabidi kuelewa vizuri kile unachofundishwa kwa kuwa kuelewa hukusaidia kukumbuka ikiwa huelewi fundisho au wazo fulani, inawezekana kwamba hutalikumbuka vizuri au hutalikumbuka kabisa. Uelewaji husaidia mtu kuelewa jinsi mambo mbalimbali yanavyohusiana na kuyaunganisha ili kupata habari inayopatana.

Jinsi unavyoweza kueleza kuhusu njia mpya ya kujifunza na kuihusianisha na maarifa ya awali, ndivyo unavyoongeza nguvu ya ufahamu wako wa kujifunza vitu vipya na zaidi unavyohusianisha mambo ndivyo inavyokusaidia kukumbuka baadaye.

Itaendelea wiki ijayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles