31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanajeshi’ mwingine JKT mbaroni

mary NzukiNA ADAM MKWEPU DAR ES SALAAM
KATIBU wa vijana waliopata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokuwa wakiandamana kushinikiza Serikali kuwapatia ajira, Rinus Emmanuel amekamatwa jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wao George Mgoba, kutekwa wiki iliyopita na kisha kupigwa na kuteswa na watu wasiojulikana.
Hata hivyo Mgoba alihamishwa kutoka Hospitali ya Amana, Ilala na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambapo anaendelea kupata mateso kutokana na kutopatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Katibu huyo alikamatwa jana akiwa na wenzake wawili wakati wakiwaongoza wenzao kwenda kumwona mwenyekiti wao, aliyelazwa katika Hospitali ya Muhimbili.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Msemaji wa vijana hao, Omary Bakari alisema katibu wao alichukuliwa ghafla na polisi walipokuwa wanaingia eneo la Muhimbili muda mchache baada ya kushuka kwenye gari.
“Hatujui nini kinaendelea hadi sasa na kwa nini polisi wanatufanyia vitendo hivi wakijua sisi si wahalifu, tunasikitika sana kwa haya yanayoendelea kufanyika juu yetu,” alisema Bakari.
Alisema pamoja na kukamatawa kwa katibu wao na watu waliodai ni askari polisi wamefuatilia kwa vyombo vinavyohusika ikiwemo polisi lakini wamekuwa wakipewa majibu ya kukatisha tama, jambo ambalo linawafanya waingiwe na hofu kuhusu hatima ya kiongozi wao.
Zaidi ya vijana 300 walikuwa wakiingia hopitalini hapo , huku baadhi yao wakiwa nyuma ghafla walishuka askari wakiwa wamevaa kiraia ambao walimvamia katibu wao na kuingia nae katika gari na kutokomea naye kusikojulina.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa vijana hao, Kiwango Mpalare, alisema kabla ya kwenda Muhimbili walikuwa na kikao chao katika Ukumbi wa Msimbazi Centre ambapo pamoja na mambo mengine walijadili hatima ya kumuuguza kiongozi wao.
“Baada ya kikao wote tulitoka na kuazimia kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kumjulia hali kiongozi wetu.
“Baada ya kufika hospitali tukiwa zaidi ya vijana 300 walikuja askari wakiwa katika gari na kumkamata katibu wetu kwa kosa la kukusanyika kinyume cha sheria. Tunajiuliza wapi tumekusanyika hali ya kuwa tulikuwa kwenye ukumbi wa mikutano.
“… je hata katika ukumbi wa mikutano napo kunahitajika kibali cha polisi, baada ya taarifa hiyo tulifuatilia polisi na kuambiwa kuwa waende wanasheria kwa ajili ya dhamana. Lakini ilishindika na wote wapo Kituo cha Polisi Cetral,” alisema Maparale.
MTANZANIA ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kiliposi Ilala, Mary Nzuki ili kupata ufafanuzi kuhusu kukamatwa kwa vijana hao alipokea simu na alipoulizwa swali aliikata.
Hata alipopigiwa kwa mara nyingine zaidi ya mara tatu simu yake iliita bila kupokewa.
Kutokana na tukio hilo alipotafutwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salam, Kamishna Suleiman Kova, alisema bado hajapata taarifa za kukamatwa kwa vijana hao ambapo aliomba afanye uchunguzi wa kina na taarifa atatoa leo.
Wiki iliyopita kiongozi wa vijana hao, Mgoba alitekwa na kisha kuteswa na watu ambao hawajajulikana, alihamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili Ijumaa jioni akitokea Hospitali ya Amana alikokuwa amelazwa awali.
MTANZANIA lilifika Muhimbili, wodi namba sita jengo la Mwaisela na kumkuta Mgoba amelazwa huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ambao walikuwa wamevalia nguo za kiraia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles