30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WANANCHI WAGAWANA MALI ZA MAGAIDI MWANZA

Ahmed Msangi
Ahmed Msangi

NA BENJAMIN MASESE,

SIKU  moja baada ya  polisi kunasa  silaha nzito za vita, mabomu yaa kurusha kwa mkono  ndani ya nyumba  moja iliyopa Bukaga Kata Kishili, wananchi wa eneo hilo wamevamia makazi hayo na  kugawana vitu vyote vilivyokuwamo na kuichoma moto.

Mwishoni  mwa wiki,  polisi wakiongozwa na Kamanda wa Mkoa huo, Ahmed Msangi, walivamia nyumba hiyo na kuwakamata watu 17 wakiwamo watoto 11 wanaodaiwa kufundishwa mafunzo ya gaidi.

Vilevile ilikamatwa bundi ya  AK 47, mabomu ya kurusha kwa mkono, visu, majambia, magazine tano zilizokuwa na risasi 150 na bunduki aina ya Mark 4 na vitu vingine.

Kutokana na hali hiyo, wananchi walivamia nyumba hiyo na kujichukulia kila kilichokuwamo na baadaye kuichoma moto huku wakidai kuwa mali hizo zimepatikana kwa damu za binadamu.

Pia wananchi hao walisisitiza kwamba kamwe hawatakubali kuona familia  au ndugu  wakijaribu kufika eneo hilo kwa kutaka kuendeleza makazi hayo.

Waliwaomba viongozi  wao kuanzia mtaa hadi kata  kuanza hatua za kuchukua kiwanja hicho kwa ajili ya kujenga ofisi ya umma na hata kituo cha polisi.

Wakati  wote tukio hilo  hakuna kiongozi wa mtaa wala kata aliyekuwapo  na kila mmoja hakutaka kutaja jina lake.

MTANZANIA ilishuhudia jinsi wananchi walivyokuwa wakivunja nyumba hiyo ambako wanaume walijikita katika kutoa mabati, milango na mageti ya chuma huku kinamama wakihaha kuchukua vitu vya ndani.

“Yaani kama unatafuta mali kwa damu ya watu, mwisho wa siku ndiyo kama haya yanakukuta, sasa kwa kuwa hizi mali zilizotokana na damu za wenzetu basi zinarudi kwa wenyewe, hatutaki familia hii au ukoo uje hapa.

“Tunaomba eneo hili lichukuliwe na Serikali kwa matumizi ya umma, hatutakuwa tayari kuona tunaishi na magaidi, tunaliomba jeshi la polisi lisiwaachie hao watu, wakija hapa tutawamaliza ,”alisikika kijana mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles